Friday, 21 November 2014

MAONYESHO YA KWANZA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DES 10 DAR




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Mmoja wa wataalamu wa hesabu, John Mataka, akitambulishwa mbele ya wanahabari (hawapo pichani)

MAONYESHO ya kimataifa ya elimu yanatarajiwa kuanza tarehe 10-14 Desemba mwaka huu, katika viwanja vya Sabasaba vya Mwalimu J. K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo yameandaliwa na kuratibiwa na Global Education Link Ltd kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Ufundi na Mafunzo na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred).

Akizungumza na wanahabari leo, maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link Ltd, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kuwatambulisha wadau wote wa elimu ili waweze kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu katika sekta hiyo. (Habari/Picha: na Gabriel Ng’osha/GPL)

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment