Hili
ndio jengo refu kuliko yote mjini Iringa. Kwa miaka mingi jengo hili
limekuwa halitumiki kwa kazi zake zilizokusudiwa. Jengo hili lina kinu
kikubwa cha kusaga na kuhifadhi nafaka. Awali lilikuwa likimilikiwa na
Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).
MAPEMA mwaka jana serikali iliamua kukikabidhi kinu hicho cha NMC Iringa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko.
Kinu
hicho chenye kiwanda cha kusaga unga, kina vienge virefu vyenye uwezo
wa kuhifadhi tani 13,500 za nafaka, na maghala mawili yenye uwezo wa
kuhifadhi tani 3,500 za nafaka na tani 1,100 ya unga.
Makabidhiano
ya kinu hicho yanayohusisha pia majengo na mali zake nyingine
yalifanyika April 10, 2011 katika hafla fupi iliyohudhuriwa na uongozi
wa mkoa wa Iringa, bodi hiyo, wafanyakazi wa NMC na wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula.
Kinu
hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakitumiki kwa kazi zake
zilizokusudiwa kilikamilika ujenzi wake mwaka 1975 uliofanywa kwa
ushirikiano kati ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania na
shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA).
Kilifunguliwa rasmi kwa ajili ya kuanza uzalishaji Julai 6, 1976 na aliyekuwa Rais wa Msumbuji Marehemu Samora Machel.
Pamoja
na kinu hicho kukabidhiwa kwa bodi hiyo, matarajio ya wakazi wengi wa
mkoa wa Iringa kwamba kingeanza kufanya kazi na kusaidia harakati za
serikali za kuongeza ajira mpya kupitia sekta hiyo ya kilimo, zinazidi
kufifia.
Kimsingi
ni kwamba hakuna kinachoendelea katika kinu hicho zaidi ya majengo yake
mengine kupangishwa kwa wafanyabiashara mbalimbali.
Wafanyabishara
hao wanaendelea na shughuli zao katika majengo ya kinu hicho pamoja na
Mwakilishi wa shirika la Consolidated Holding Corporation (CHC)
lililochukua nafasi ya shirika la Kurekebisha Mashirika ya Umma, Joseph
Mapunda kuahidi kwamba wangepewa notisi baada ya makabidhiano hayo.
Wapangaji
walio katika majengo ya kinu hicho ni pamoja na wakala wa kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), wakala wa safari za anga, Bar maarufu ya Dragon na
ofisi za wadau mbalimbali.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment