Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Friday, 28 November 2014

PENNY AFUNGUKA: SIWEZI KUVUNJA USHOSTI WA WEMA, AUNT!



Stori: IMELDA MTEMA

MTANGAZAJI Bongo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kuwagombanisha marafiki wa damu, Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel, baada ya yeye kuingilia urafiki huo.Mtangazaji Bongo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akiwa na Wema Sepetu.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Penny alisema kuwa anaamini kabisa kuna baadhi ya watu hawapendi kuwa na urafiki zaidi ya watu watatu kitu ambacho siyo sahihi, yeye anaamini baada ya kupatana na Wema hivi karibuni, watakuwa marafiki watatu.

Wema Sepetu akiwa na Aunty Ezekiel.

“Nafurahi sana tunapokuwa na kampani kubwa nashangaa wengine mpaka wanafikia kupigana kisa akiona rafiki yake ana urafiki na mtu mwingine, mimi napenda tuwe wengi ili tuweze kushauriana mambo mbalimbali,” alisema Penny.

HAMISA ABWATUKA KISA MABUZI




Stori:MUSA MATEJA

MWANAMITINDO kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto amepangua tuhuma ambayo amekuwa akitupiwa na watu wanaomuona aking’aa kisha kudai anatumia mgongo wa wanaume tofautitofauti (mabuzi).

Mwanamitindo kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Hamisa alisema amekuwa akisikitishwa na tabia hiyo ya watu kumnanga kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatupia picha nyingi ili kujiuza kwa mabuzi kitu ambacho si cha kweli.

“Kiukweli asiyekujua hakuthamini, nasema hivi kutokana na watu wengi wamekuwa wakinisema vibaya hasa katika mitandao ya kijamii, wanikome kwani kila mtu ana maisha yake na mimi sitegemei mabuzi kuishi mjini, nina mpenzi wangu mmoja tu,” alisema Mobeto.

AUNTY LULU ASIMULIA ALIVYOBAKWA




Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan

My confession! (kukiri kwangu)! Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefungua kinywa na kutoa la moyoni akisimulia tukio baya lililowahi kumkuta la jinsi alivyobakwa, Risasi Jumamosi lina ‘exclusive story’.

Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipozi.

TUJIUNGE DUKANI KWAKE
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni dukani kwake Kinondoni jijini Dar, Aunty Lulu asiyeishiwa na vimbwanga alisema kwamba, kamwe hawezi kusahau tukio hilo maishani mwake.

ALIBAKWA NA RAFIKI WA SHEMEJI YAKE
Aunty Lulu aliyeng’ara kwenye Sinema ya Lost Soul alieleza namna alivyobakwa na rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) na kumpotezea ndoto zake za kuanza mchezo huo akiwa ndani ya ndoa.

Akieleza kwa uchungu na masikitiko, Aunty Lulu alitiririka kwamba, alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi maeneo ya Posta jijini Dar.

KISUTU SEKONDARI
Aunt Lulu alisema kwamba wakati huo, yeye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Kisutu, Dar, hivyo kila siku jioni mwanaume huyo alikuwa akimpitia na kumpa lifti hadi nyumbani.
Aliendelea kusema kwamba, siku moja jamaa huyo aliyekuwa amemzidi umri maradufu alimtaka wafanye mapenzi lakini alimkatalia kwa madai kwamba hakuwahi kufanya mchezo huo mbaya ambao alifundishwa kuwa ni dhambi.

TUKIO BLOCK 41
“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri, nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni) ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,” alisema Aunty Lulu, mtangazaji wa zamani wa ITV na C2C.

Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ akiwa dukani kwake.

MAUMIVU MAKALI
Staa huyo aliendelea kutiririka kwamba alipomwambia kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho, mwanaume huyo alimwambia haamini ndipo akamkamata kinguvu na kumpeleka chumbani kwake kisha akamwingilia na kumsababishia maumivu makali. “Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.

AGOMA KUTAJA MWANAUME
“Ilibidi dada anibane kujua nina tatizo gani. Kwa kuwa nilikuwa sina ujanja nilimwambia nimeingiliwa kwa mara ya kwanza lakini nilisita kumtaja mwanaume huyo.
“Dada aliponibana sana nilimwambia kwamba niliingiliwa na huyo rafiki wa mume wake.

INASIKITISHA
“Lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na ukweli liliwaumiza sana dada na shemeji yangu.
“Walimsema sana mwanaume huyo na ikawa ndiyo mwisho wa urafiki wao.

ALIKUWA NA UMRI GANI?
“Umri sikumbuki lakini nakumbuka nilikuwa nakaribia kuingia kidato cha nne. Yule mwanaume alizoea kuninunulia vifaa vya shule na kunisisitiza kusoma.

“Nilimuona mtu bora sana, nikamzoea na ikawa rahisi kwenda kwake kusoma maana jamaa alikuwa ‘jiniazi’ na mwanzoni alikuwa jirani yetu kabla ya kuhama.
“Ukweli huwa sipendi kuelezea historia ya maisha yangu ya mapenzi kwani inaniumiza sana.

AMPOTEZEA NDOTO YA KUOLEWA
“Huwa najisikia kulia kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.
“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu.

YUPO WAPI MWANAUME HUYO?
“Baada ya tukio lile aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume wasiowajua kiundani,” aliweka nukta Aunty Lulu.

Thursday, 27 November 2014

UFANYEJE MWENZI WAKO ANAPOKOSA HAMU YA TENDO.......




Uhali gani mpenzi msomaji wa kona hii mahususi kwa ajili ya wapendanao, ni matumaini yangu kwamba uko poa na unaendelea fresh na majukumu ya kila siku. Ni wiki nyingine tunapokutana katika uwanja wetu huu, kujadili mambo mbalimbali yahusuyo sanaa ya mapenzi.

Wiki iliyopita tulianza kujadili mada hii ya mbinu za kufanya ili kumsaidia mwenzi wako aliyepoteza hamu ya tendo la ndoa. Nilichokigundua ni kwamba wengi wanasumbuliwa na tatizo hili lakini hawana pa kusemea wala hawajui wafanye nini.

NINI CHA KUFANYA?
Baada ya wiki iliyopita kuangalia jinsi tatizo la kukosa hamu ya tendo kwa mwanamke linavyotokea na dalili zake, leo tuangalie mbinu za kufanya mwenzi wako anapokuwa katika hali hii ili kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida.

Kama nilivyosema awali, zipo sababu nyingi zinazosababisha hisia za mwanamke kuisha na kupoteza kabisa hamu ya kukutana faragha na mwenzi wake.

Tuliona jinsi migogoro ya kimapenzi, msongo wa mawazo, pilika za maisha na kushindwa kutoshelezwa kwenye tendo kunavyosababisha wanawake wengi kupoteza hamu ya kukutana na wenzi wao faragha.
Ili kukabiliana na tatizo hili, ni vizuri kuanza kushughulikia sababu zilizomfanya mwenzi wako akafikia kwenye hatua hiyo mbaya.

1. SHUGHULIKIA MIGOGORO YA KIMAPENZI
Endapo kuna tatizo limetokea kati yako na mwenzi wako, kwa mfano mwenzi wako anahisi unamsaliti kwa kutoka na mwanamke mwingine, humshirikishi kwenye mipango ya familia, hajui hata mshahara wako ni kiasi gani na unatoka lini, unaleta ubabe ndani ya nyumba, unachelewa kurudi nyumbani bila sababu, humtoi ‘out’ wala humnunulii zawadi, atahisi humpendi.

Atabaki na vinyongo na manung’uniko ndani ya moyo wake na taratibu ataanza kupoteza hisia za mapenzi juu yako. Ni lazima kila mgogoro unapotokea, ukashughulikiwa kwa busara ili kila mmoja aridhike na kuondoa dukuduku ndani ya moyo wake.

Wanawake wengi ni mahodari wa kukaa na vinyongo ndani ya mioyo yao hivyo kama mwanaume hujui namna ya kumaliza kabisa matatizo, umpendaye ataishia kwenye hali ya kupoteza hamu ya kuwa na wewe faragha. Mpe nafasi mwenzi wako azungumze hisia zake na hiyo itamsaidia kutoa vinyongo na manung’uniko.

2. MSAIDIE KUPAMBANA NA MSONGO WA MAWAZO
Njia nzuri ya kupambana na ‘stress’ zinazosababishwa na kazi, ni vizuri wanaume kuwa wanaelewa nini wenzi wao wanahitaji wanapotoka kazini. Hii inawahusu zaidi wanawake wanaofanya kazi kwani wengi wao wanaongoza kwa kupoteza hamu ya tendo kutokana na matatizo wanayokutana nayo kutwa nzima wakiwa kazini.

Zungumza kwa upole na mwenzi wako akirudi kutoka kazini, muulize jinsi siku yake ilivyokuwa, muulize mambo yaliyomkwaza kwa siku nzima na yale yaliyomfurahisha. Mpe pole kwa kazi, mtie moyo pale alipokosea na mfanye ayaone matatizo ya kazini kuwa sehemu ndogo ya maisha yake.

Hiyo itamfanya ajihisi kuwa kwenye mikono salama na atasahau kero zote alizokutana nazo kutwa nzima, hata mkipanda kitandani, atakuwa mtu mpya na atafurahia kuwa na wewe faragha. Kama kazi anazofanya zinahusisha mwili kuchoka, si vibaya kama ukamfanyia mkeo ‘masaji’ ya kupunguza uchovu.

Wengi wanaamini kwamba wanaume ndiyo watu wa kufanyiwa vitu hivyo tu, la hasha, hata wanawake nao kuna muda wanahitaji ili kurudi kwenye utulivu wa kihisia.

PICHA ZA RECHO ZAMZUIA SAGUDA MAMBO YA MAPENZI




Stori: Gladness Mallya
ALIYEKUWA mchumba wa msanii wa filamu Bongo, marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Saguda amefunguka kuwa picha za mwanadada huyo zimekuwa zikimfanya asiwe na hisia za kuwa na mwanamke mwingine.

George Saguda akiwa na aliyekuwa mchumba wake marehemu Sheila Haule ‘Recho’.

Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, Saguda alisema tangu mchumba wake huyo afariki dunia hajawahi kuwa na mwanamke na hana mpango huo kwa sasa labda hapo baadaye.

“Tangu alipofariki Recho niko peke yangu na sina mpango wa kuwa na mwanamke mwingine, kwani kila ninapozitazama picha zake naumia sana,” alisema Saguda.

Saguda aliongeza kuwa, licha ya kwamba yeye ni mwanaume aliyekamilika lakini tangu mchumba wake alipofariki dunia hana hisia za kimapenzi kwa mwanamke mwingine na akipata hali hiyo huzitazama picha zake hisia hizo hutoweka.

Wednesday, 26 November 2014

PATI YA BETHIDEI YA BABY MADAHA UCHAFU 85%





Stori: Issa Mnally
SHEREHE ya siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki na filamu, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ilitawaliwa na vitendo vichafu mwanzo mwisho.

Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiogeshwa pombe na mashosti zake.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wachache wakiwemo baadhi ya wasanii, ilifanyika katika Grosari moja iliyopo Kijitonyama.Miongoni mwa mastaa waliohudhuria alikuwa ni mcheza soka wa zamani wa timu ya Yanga ya jijini Dar, Samson Mwamanda.

Sherehe hiyo iliyoanza mishale ya saa 6.00 usiku ilitawaliwa na vituko kibao vilivyowaacha midomo wazi baadhi ya wahudhuriaji.Moja ya vituko hivyo ni pale Baby Madaha aliyekuwa amekolea kwa kilevi alipoamua kupigana denda laivu na msanii Isabela Mpanda ambaye naye alikuwa kachangamka ile mbaya.

Baby Madaha akifurahia bethidei na shosti yake Isabela.


Isabela alikuwa kituko zaidi kufuatia kuvaa kinguo kifupi cha pinki kilichoacha sehemu kubwa ya mwili wake, hasa kuanzia mapajani kuwa wazi.

Msanii huyo pamoja na kujitupa huku na huko kilevi na kucheza muziki kwa kukata nyonga kinoma, alikuwa akiinua nguo yake juu na kuonesha kufuli lake ‘white’ na kujishika sehemu za nyuma jambo lililomfanya mmoja wa wahudhuriaji kusema:

Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiwa amelowa pombe. “Jamani pombe ni noma, mnaona mambo ya aibu anayoyafanya Isabela?”
Kituko kingine ni pale mastaa hao waliokuwa bwii kwa kilevi akiwemo Mwamanda, walipoamua kummwagia pombe kichwani na kwenye nguo zake Baby Madaha baada ya kumuimbia wimbo wa ‘Happy birth day to you…!

Tuesday, 25 November 2014

breaking news.... CHOKI KUOA SOON




Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
MIEZI michache baada ya kufiwa na mkewe, aliyejulikana kama Mama Shuu, Mkurugenzi wa Extra Bongo ‘Next Level’, Ali Choki amesema kutokana na kuishi na familia, atalazimika kuoa tena ‘very soon’.

Mkurugenzi wa Extra Bongo ‘Next Level’, Ali Choki

“Nitaoa hivi karibuni maana nitaepukana na vishawishi na mambo mengine, pia mimi kama mwanaume siwezi kukaa peke yangu ukizingatia nina watoto wanahitaji mtu wa kuwaangalia, nilikuwa nimemzoea mke wangu lakini ndiyo hivyo ameniacha na maisha lazima yaendelee,” alisema Choki.

Mama Shuu alifariki miezi miwili iliyopita baada ya kuandamwa na maradhi kwa kipindi kirefu. Katika hali nyingine, Choki aliwabeza wanaodai kwamba bendi yake itatetereka kutokana na kifo hicho na kudai kuwa ‘wanaongea wasichokijua’.

Monday, 24 November 2014

DEAR, MPENZI: MANENO YASIYOKUWA NA MAANA TENA





NI Jumanne tena! Nawakaribisba wasomaji wangu wa safu hii makini kwa elimu ya mapenzi katika maisha.Wiki iliyopita tulikuwa na mada ya ‘wengi wanapenda harusi kuliko ndoa’. Wenye kuelewa walielewa.Wiki hii nina mada nyingine kabisa inayosema dear, mpenzi ni maneno yasiyokuwa na maana tena.

Hapa namaanisha kwamba, miaka ya zamani, wapendanao au wapenzi waliyatumia sana maneno haya katika kuoneshana upendo wa dhati.
Ilikuwa sifa kubwa kumsikia msichana akimwita boyfriend wake ‘dear’au mpenzi!
“Niambie my dear! Upo mpenzi?” ndivyo ilivyokuwa.

WAMEANZA KUHARIBU WANAWAKE
Mara ya kwanza nilishangaa kumsikia mwanamke mmoja kwenye simu anamwita mwanamke mwenzake dear. Tena alisema: my dear, zile sabuni za kuondoa alama nyeusi usoni ulizinunua wapi?”
Kuna siku nilimsikia mwanamke mwingine kwenye simu akisema: “Nakuja mpenzi wangu jamani. Kwanza we umebeba na kile kitenge nilichokuagiza?”

AKILINI MWANGU
Awali niliamini wanaozungumza nao kwenye simu huenda ni wanaume, lakini meseji zilionesha upande wa pili ni wanawake wenzao. Kwa maneno ya sabuni za kuondoa alama nyeusi usoni na kitenge.

LIMESAMBAA
Baada ya hapo nilianza kufuatilia hatua kwa hatua nikaja kubaini waziwazi kwamba, wanawake wengi wameshapoka maneno hayo kutoka kwenye kuyatumia kwa wapenzi wao na kuwapachika mashoga zao.

MADHARA YAKE
Nilichobaini kwa harakaharaka siku hizi ni kwamba, baadhi ya wake za watu wamekuwa wakibebeshwa sifa ya umalaya kwa sababu ya matumizi ya maneno haya mawili. Mfano, mke wa mtu yuko ndani kwake, anapokea simu ya mwanamke mwenzake, anasema: Niambie my dear... we umefika kwani...basi na mimi naoga nakuja...haya mpenzi wangu nakuja sasa hivi.

Kwa majirani wanaomsikia mwanamke huyo, baadhi yao huamini alikuwa akizungumza na mchepuko kwa sababu ya my dear na mpenzi.

HAYANA MAANA TENA

Wiki iliyopita niliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wanaume ambao wanafahamu kuhusu wanawake kuyatumia maneno hayo mawili kwa kuitana wenyewe.

Maoni yao yalisimama kwenye maana moja kwamba, maneno hayo kwa sasa hayana maana tena katika matumizi ya wapendanao.
“Sasa kama mke wangu anamwita mwanamke mwenzake dear au mpenzi, akiniita mimi kuna maana gani? Yaani mimi na shoga yake ni kitu kimoja?” alihoji baba Abdul, mkazi wa Mabibo jijini Dar.

Baba Steve wa Sinza-Mori, Dar: “Kusema ukweli wanawake wanavuruga mambo mengi sana ila hatujui tu. Ukiachilia mbali hayo maneno kuyatumia kuitana wenyewe kwa wenyewe we si unaona siku hizi kila mmoja anavaa suruali.”

“Ah! Mimi niliwahi kumuuliza mke wangu ni kwa nini anamwita mwanamke mwenzake dear, akasema haoni tatizo, lakini ukweli mimi naona tatizo lipo. Ipo siku na mimi nitampigia simu rafiki yangu anaitwa Sudi nitamwita honey, nimsikie mke wangu atasemaje,” alisema Abdallah Mkadala, mkazi wa Buguruni, Dar.

NI MBINU YA USALITI?
Baadhi ya wanaume walionesha wasiwasi wao kwamba, huenda wanawake wanaitumia fursa hiyo kuweza kusaliti!

Kivipi? Kumbe inawezekana mwanaume akakaa na mpenzi wake ambaye anaweza kupokea simu ya mchepuko akatumia neno dear au mpenzi kwa kumaanisha huku mwanaume huyo akijua anaongea na mwanamke mwenzake!

WANAWAKE WENYEWE WANASEMAJE?
Pia niliweza kuzungumza na baadhi ya wanawake kuhusu matumizi ya maneno hayo. Niliwalenga zaidi wale wanaopenda kuyatumia.

Mama Mwamtumu wa Makongo, Dar: “Kusema ukweli wanawake tumeshajiweka kwenye mazoea, hasa sisi wa mijini. Lakini kiusahihi kabisa si maneno mazuri kuyatumia sisi kwa sisi japokuwa maana ya maneno yenyewe ni upendo tu.”

Skola, mkazi wa Bunju B: “Dear na mpenzi ni neno moja jamani! Ni kuonesha upendo kwa mwenzako. Ila ni kweli kuna ukakasi. Mfano wanaume nao wakiamua kuitana sweet, darling naamini sisi wanawake hatutawaelewa hata kidogo.”

Saturday, 22 November 2014



KAJALA KUZAA TENA!
 

Stori: Imelda Mtema
MWIGIZAJI Kajala Masanja amefunguka kuwa anatamani kuongeza mtoto wa pili kwani tayari aliyenaye ameshakua vya kutosha.

Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Kajala alisema anasaka mimba kwa namna yoyote ili mwanaye Paula apate mdogo wake hivyo suala hilo lipo katika mchakato yakinifu na mpenzi wake wa sasa ambaye hakupenda kumwanika jina lake.

Kajala Masanja akipozi.

“Natamani kuongeza mtoto wa pili, Paula ameshakua mkubwa lazima tumtafutie mdogo wake mambo ndiyo yatakuwa mazuri zaidi,” alisema Kajala.Mtoto huyo wa awali, Kajala alizaa na prodyuza Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye walishamwagana.

Friday, 21 November 2014

HAUMUAMINI, UNAISHI NAYE KWA MACHALE, MAANA YAKE NINI? JIONGEZE!




NIMEFURAHI tumekutana tena katika safu yetu hii tunapata kujuzana masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.Ni mambo ya mahaba, hujakosea. Hapa tunaongeza maarifa ya mapenzi kila uchwao, karibu.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Natambua wengi tu wanaishi kwenye uhusiano wa namna hii.

Utakuta mtu anaishi kwa muda mrefu na mwenzake pasipo kuwa na imani naye. Anakuwa mguu ndani mguu nje kwamba yupo tayari kwa lolote, muda wowote.Eti anaamua kwamba bora penzi lake liende bila ya kuwa na malengo ya baadaye kwani hamuamini mpenzi wake.

Mtu wa aina hiyo mara nyingi anakuwa na hofu ya kupenda moja kwa moja kwa kuhofia kwamba asije akaambulia maumivu pale atakapozama moja kwa moja penzini.Unapokosa imani na mtu kwenye uhusiano ni hatari maana mapenzi yanajengwa na imani. Wapendanao lazima waaminiane, imani ikitoweka hakuna mapenzi.

Uaminifu unaanzia kwenye urafiki, uchumba na hata pale mtakapofikia katika hatua ya kuoana.
Imani inapopotea kwa marafiki, wachumba au wanandoa huwa kinachofuata penzi kusambaratika. Huwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba ambaye haumuamini.Kukosa imani na mtu ambaye pengine unahitaji apite kwenye hatua za kuwa mchumba au kuwa mke na mume kuna madhara mengi lakini haya hapa chini ni baadhi:

KUTOFURAHIA PENZI
Imani inapokuwa haipo kwa mpenzi wako, kamwe hautoinjoi mapenzi. Utakuwa mtu wa hofu kila wakati badala ya kuipa nafasi furaha, kila wakati utawaza mambo mengi kwenye akili yako. Badala ya kufurahi faragha, wewe utawaza kusalitiwa.

Simu ikiingia katika simu ya mpenzi wako wewe tayari roho juu. Akili yako inakwenda mbali na kuhisi labda ni mchepuko wake. Wewe utakuwa ni mtu wa presha mwanzomwisho. Mapenzi matamu unakuwa unayasikia kwa wengine.

KUPOTEZA MUDA
Wakati unaishi kwa machale, muda nao siku zote huwa haumsubiri mtu. Miaka inaendelea kusonga huku wewe ukiendelea kudumu katika penzi ambalo halina mbele wala nyuma. Wakati wenzako wakifanya maamuzi sahihi ya kuingia kwenye ndoa wewe utakuwa unaishi kwa mashaka.

Kila siku utakuwa ukisogeza mbele uamuzi wa kuoana na mpenzi uliyenaye maana unaona muda bado wa kufanya maamuzi hayo, eti unasema ngoja umpe muda kidogo pengine kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, utamuamini. Kila siku unasema labda kesho kumbe miaka inazidi kukatika.

MALIPIZI
Umpendaye akigundua kwamba haumuamini, naye ataishi na wewe katika staili ya kutokuamini. Atakudanganya kama anakupenda kumbe moyoni naye hakupendi. Ni rahisi wakati huo na yeye kutumia nafasi hiyo kuanzisha uhusiano na mtu mwingine huku wewe akikufanya kama akiba. Ataanzisha uhusiano na mtu ambaye anaamini kwamba naye anamuamini. Hatakubali kubaki na wewe peke yako huku akiamini kabisa humuamini na unaishi kwa machale

Tuesday, 18 November 2014

soma story mzima... AMFUMANIA MUMEWE, ASAULA!



Stori: Waandishi Wetu
HATARI! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine.

Mwanamke anayejulikana kwa jina la Tatu Ikoko akitishia kusaula mbele ya watu.

Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.

“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani, akaanzisha vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.

Tatu Ikoko akiwa katika hali ya kuvurugwa baada ya kumfuma mumewe na hawara.

“Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake walimshika na kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo na waliachana kwa tabia hiyo.

Majirani wakimsitiri Tatu Ikoko.

“Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,” kilisema chanzo hicho.imeandikwa na shani ramadhani na mayasa mariwata.

Sunday, 16 November 2014

jamani hii noma... AUNT LULU AKIRI MASTAA KUJIUZA MITANDAONI




Mwanadada mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’

MWANADADA mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameibuka na kueleza kwamba mastaa wamegundua njia mpya ya kujiuza ambayo ni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akistorisha na gazeti hili, Aunt Lulu alisema mastaa wengi wa kike wanajiuza kwenye mitandao ambapo mapedeshee waliopo mikoa mbalimbali wakishaziona picha zao huwa wanawatafuta kwa udi na uvumba ambapo wanawapigia simu na kuwatumia fedha na tiketi za ndege ya kwenda na kurudi.

‘Aunt Lulu’akiwa kwenye pozi.

“Yaani mastaa wa kike hatulali unakuta pedeshee anakutumia tiketi ya ndege unamfuata mkoani ukienda usiku asubuhi umesharudi Dar unaendelea na mambo yako ndiyo maana unawaona wasanii wengi wa kike wana fedha lakini kazi wanazozifanya huzioni,” alisema Aunt Lulu.

eeeeeeeeeeeee...... UMUHIMU WA KUTOKA OUT NA UMPENDAYE



Nianze kwa kumshukuru Maulana kwa kutuwezesha kuiona salama siku ya leo, ni matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko vizuri na unaendelea kulisongesha mbele gurudumu la maendeleo.
Wiki iliyopita tulianza kujadili mada juu ya umuhimu wa kutoka ‘out’ na umpendaye. Tuliona jinsi kutoana out kunavyoweza kufufua mapenzi kati ya wawili wapendao bila kujali wameishi kwa muda gani katika uhusiano wa kimapenzi.

Tuendelee na sehemu ya pili ya mada yetu ambapo tutazungumzia mambo ya muhimu ya kuzingatia mnapotoka ‘out’ na yale ambayo hutakiwi kabisa kuyafanya unapotoka na umpendaye.

1. MAANDALIZI
Unapopanga kutoka na umpendaye, ni vizuri kufanya maandalizi ya kutosha ya vitu vyote muhimu ili siku ikifika, isionekane umekurupuka. Ni vizuri kufanya maandalizi ya sehemu unayotaka kumpeleka mwenzi wako na kuhakikisha ina utulivu wa kutosha na usalama.

Baada ya kuwa na uhakika na sehemu mtakayoenda, ni vizuri kujiandaa wewe binafsi. Andaa nguo safi, fanya usafi wa mwili ikiwa ni pamoja na kuoga vizuri na kupiga mswaki kwani mkiwa out, lazima mtasogeleana na mwenzi wako hivyo kama unanuka mdomo au jasho, unaweza kuwa kikwazo kwa mwenzi wako.

Hata kama hatakwambia, hatafurahia kuwa na wewe karibu. Unaweza pia kujipulizia marashi mazuri yatakayoongeza bashasha.

2. MPE KIPAUMBELE
Baada ya maandalizi ya awali kuwa yamekamilika, jitahidi kuwahi kabla ya muda mliokubaliana. Akifika na kukukuta tayari umeshafika na kumsubiri, ataona umempa kipaumbele, jambo litakalomfurahisha. Mpokee kwa uchangamfu, inuka, muoneshe sehemu ya kukaa na akishakaa na kutulia, na wewe kaa kisha muulize kitu atakachokipendelea.

Anzisha mazungumzo ya kawaida huku ukijitahidi kuwa na tabasamu kwenye uso wako kwani kuna usemi wa wahenga kwamba tabasamu ni kama uchawi wa kimapenzi, hata kama mwenzi wako ana hofu ndani ya moyo wake, akikuona umetabasamu, atatulia na kufurahia kuwa pamoja na wewe.

3. EPUKA MATUMIZI YA SIMU
Watu wengi huwa wanakosea jambo moja, unakuta bibi na bwana wametoka ‘out’ lakini kila mmoja yuko bize na simu yake. Mwanaume yuko bize kuchat Whatsapp au Facebook, mwanamke yuko bize Instagram au kutuma meseji za kawaida.

Nakushauri msomaji wangu usiwe na tabia kama hii kwani haileti picha nzuri. Ikiwezekana, zima kabisa simu yako au itoe mlio ili akili yako yote uielekeze kwa mwenzi wako. Utajisikiaje pale unapomwambia mwenzio kitu kizuri lakini kumbe wala hakusikilizi yuko bize na simu yake? Haileti picha nzuri.

4. EPUKA MATUMIZI YA POMBE KUPITA KIASI
Kama wewe ni mtumiaji wa kilevi, jizuie kunywa hadi kulewa wakati ukiwa kwenye mtoko na mwenzi wako. Kwa kawaida, mtu aliyelewa, hawezi kuzungumza kwa busara, anaweza kufanya jambo lolote la aibu bila kujijua na hawezi kuwa makini katika mazungumzo. Epuka kulewa ukiwa out na mwenzi wako.

5. ZUNGUMZA KWA BUSARA
Badala ya wewe kuwa mzungumzaji mkuu, washauri wa mambo ya mapenzi wanaeleza kwamba ni lazima uongozwe na busara katika kila unachokizungumza. Achana na habari za wapenzi wako waliopita, zungumza naye mambo mazuri ikiwemo mipango ya maisha ya baadaye na jitahidi kuwa msikilizaji kuliko mzungumzaji.

Ni matumaini yangu kwamba ukizingatia haya, utafanikiwa ‘kumroga’ mpenzi wako, ataendelea kukupenda na muda mwingi atakuwa akikufikiria wewe pamoja na kukumbuka mambo mazuri mliyoyafanya pamoja mkiwa out.

Thursday, 13 November 2014

AIBU! PICHA ZA JACK DUSTAN AKIOGA BAFUNI ZAVUJA



Stori: Imelda Mtema
Msanii wa filamu ambaye sasa amejichimbia Dubai akisaka maisha, Jacqueline Dustan amevujisha picha zinazomuonesha akioga bafuni huku akionekana yuko bwii, jambo ambalo ni kinyume na maadili.

Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Dustan akioga huku akinywa.

Picha hizo zinamuonesha msanii huyo akiwa kwenye sinki lenye mapovu na nyingine zikimuonesha hadi sehemu zake muhimu.

Hizi ni picha zikionyesha Jacqueline Dustan akioga kwa kujiachia.


Katika kutaka kupata sababu ya mwanadada huyo kuziachia picha hizo ambazo Ijumaa imezipata kutoka kwa rafiki yake wa karibu (jina tunalihifadhi) ikidaiwa kuwa aliyempiga ni bwana wake, mwandishi wetu alimtafuta kupitia simu yake ya kiganjani na alipopatikana alisema: Cha ajabu kipi hapo, nilikuwa naoga kwa raha zangu nikamuita mtu akanifotoa, tatizo liko wapi?”

LULU AFUNGUKA KUWA HAPENDI KUWA KATIKA UHUSIANO WA MAPENZI




Stori: Imelda Mtema

Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.

Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi..

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.

“Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa, hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,” alisema Lulu.

Wednesday, 5 November 2014