Tuesday, 25 November 2014

breaking news.... CHOKI KUOA SOON




Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
MIEZI michache baada ya kufiwa na mkewe, aliyejulikana kama Mama Shuu, Mkurugenzi wa Extra Bongo ‘Next Level’, Ali Choki amesema kutokana na kuishi na familia, atalazimika kuoa tena ‘very soon’.

Mkurugenzi wa Extra Bongo ‘Next Level’, Ali Choki

“Nitaoa hivi karibuni maana nitaepukana na vishawishi na mambo mengine, pia mimi kama mwanaume siwezi kukaa peke yangu ukizingatia nina watoto wanahitaji mtu wa kuwaangalia, nilikuwa nimemzoea mke wangu lakini ndiyo hivyo ameniacha na maisha lazima yaendelee,” alisema Choki.

Mama Shuu alifariki miezi miwili iliyopita baada ya kuandamwa na maradhi kwa kipindi kirefu. Katika hali nyingine, Choki aliwabeza wanaodai kwamba bendi yake itatetereka kutokana na kifo hicho na kudai kuwa ‘wanaongea wasichokijua’.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment