Showing posts with label MUSIC. Show all posts
Showing posts with label MUSIC. Show all posts

Monday, 24 November 2014

KALA JEREMIAH AFANYA UZINDUZI WA VIDEO NA AUDIO YA WIMBO YAKE MPYA YA “USIKATE TAMAA”



Kala Jeremiah akichana mistari.
Mwanamziki wa Hip hop, Kala Jeremiah amezindua video yake ya Wimbo Usikate Tamaa aliomshirikisha Nuruwell katika Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Katika uzinduzi huo, Kala alisindikizwa na mastaa kibao wakiwemo Mo Music, Ben Pol, La Veda, Stamina, Ney Lee ambao waliporomosha shoo za nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo. Kala Jeremiah amesema audio na video zinatarajia kutoka rasmi siku ya Jumatano yaani tarehe 26/11/2014.(Picha na Pamoja Blog)

Kala Jeremiah akiendelea kufanya ya kwake kwenye stage wakati wa uzinduzi video ‘Usikate Tamaa’

Stamina akizidi kutiririsha mistari kwa mashabiki wake.

Sunday, 23 November 2014

KALA JEREMIAH, LA VEDA, MO MUSIC, BEN POL, STAMINA, NEY LEE WAFUNIKA UZINDUZI WA VIDEO 'USIKATE TAMAA'







Kala Jeremiah (kushoto) na Nuruwell wakipafomu kwa mara ya kwanza wimbo wa Usikate Tamaa ndani ya Maisha Club.



Kala Jeremiah akikamua sambamba na Ney Lee kabla ya kuzindua video yake ya Usikate Tamaa.



Nuruwell akiimba kwa hisia wakati wa uzinduzi wa video ya Usikate Tamaa.



Kala Jeremiah akichana mistari.



Ney Lee akiimba kwa hisia kali.



Mshiriki wa Big Brother Hotshots, Irene La Veda akionyesha ufundi wa kutumia saxaphone ndani ya Ukumbi wa Miasha Club usiku wa kuamika leo.



La Veda akizidi kufanya yake stejini.



La Veda akipafomu wimbo wake mpya wa 'Let It Go' kwa mara ya kwanza.



Mwanamuziki Mo Music akitoa burudani katika kusindikiza uzinduzi wa video mpya ya Kala Jeremiah.



Mo Music akizidi kuwadatisha mashabiki ndani ya Maisha Club.



Ben Pol akiwapa raha mashabiki wa Maisha Club usiku wa kuamkia leo kabla ya uzinduzi ya video 'Usikate Tamaa'.



Ben Pol akiendelea kufanya yake stejini.



Mwana Hip hop, Stamina akifanya vitu vyake stejini.



Stamina akizidi kutiririsha mistari kwa mashabiki wake.



Kalla akimtambulisha prodyuza aliyetengeneza wimbo wake mpya wa Usikate Tamaa kwa mashabiki.



Kalla akiwatambulisha pia walioshiriki katika video ya wimbo wake huo wa Usikate Tamaa aliomshirikisha Nuruwell.



Kala akipozi katika bango la Pepsi ambao ni wadhamini wa uzinduzi wa video yake.



Kala Jeremiah na Mo Music wakipozi na mashabiki wao.

MWANA Hip hop, Kala Jeremiah amezindua video yake ya Wimbo Usikate Tamaa aliomshirikisha Nuruwell katika Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Katika uzinduzi huo, Kala alisindikizwa na mastaa kibao wakiwemo Mo Music, Ben Pol, La Veda, Stamina, Ney Lee ambao waliporomosha shoo za nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo.

Video ya wimbo huo itaingia mtaani rasmi Jumatano hii ambapo mashabiki na wapenzi wa muziki wataipata kupitia mitandaoni.

Tuesday, 18 November 2014

SKYMOTO YAWABAMBA WAKAZI WA JIJINI MWANZA NDANI YA JEMBE BEACH




Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akizungumza na wakazi wa Mwanza kuwakaribisha kwenye show ya SKYMOTO iliyofanyika kwenye hekalu la maraha la Jembe Beach lililopo Malimbe jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akimtambulisha Mkurugenzi wa Yamoto Band Said Fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe kwa wakazi wa jijini Mwanza waliotinga kwenye hekalu la maraha lililo Malimbe jijini Mwanza Jembe Beach.


Vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza wakifungua burudani kwa kumpa sapoti Digna Mbepera (wa pili kulia) kutoa burudani kwa wakazi na mashabiki wa Skylight Band mwishoni mwa juma. Kutoka kushoto ni Sony Masamba, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Hashim Donode (kulia).



Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na Digna Mbepera wakionyesha ufundi wao ndani ya Jembe Beach.

Rapa mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower (kushoto) akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza kwenye show ya aina yake iliyopewa jina la SKYMOTO huku wakikolabo na Yamoto Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.

Raia wa kigeni na couple yake wakiburudika na burudani kutoka vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.

Kikosi kazi cha Skylight Band kikishambulia jukwaa kwa manjonjo ya aina yake.

Sam Mapenzi wa Skylight Band akiwa raha wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach mwishoni mwa juma walipo kolabo na Yamoto Band.


Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na Skylight Band ndani ya Jembe Beach.




Aneth Kushaba AK47 akiwa chezesha ligwaride wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.

Sam Mapenzi, Aneth Kushaba na Digna Mbepera wakishambulia jukwaa.

Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa jijini Mwanza waliofurika kwenye show ya SKYMOTO ndani Jembe Beach.



Dogo Asley akiongoza Yamoto Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza walipofanya kolabo na Skylight Band kuwapa raha wakazi wa jijini Mwanza.

Yamoto Band wakishambulia jukwaa ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza mwishoni mwa juma.

Yamoto Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.

Yamoto wakimwaga mauno kwa mashabiki wa wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach.

Wadau wengine watulia karibu na kaunta ya vinywaji ya Jembe Beach huku wakiburudika na burudani ya Skylight Band kwa mbali wakichochea mzuka wa kucheza.

Pichani juu na chini mashabiki wakiwa wamefurika kenywe bustani ya Jembe Beach kushuhudi burudani ya Live Music kati ya Yamoto Band na Skylight Band show ya iliyopewa jina la "SkyMoto" maalum kwa mashabiki wa jijini Mwanza.
Kwa picha zaidi ingia hapa

Wednesday, 12 November 2014

breaking news..... MWANAMUZIKI GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA




Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' enzi za uhai wake.

MWANAMUZIKI wa Hip Hop nchini, Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' amefariki dunia jana usiku akiwa mkoani Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita akitokea jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bwana Dennis ambaye alikuwa mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha kuhusu kifo hicho na kusema rapa huyo aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya. Marehemu Geez Mabovu anatarajiwa kuzikwa leo Novemba 13, 2014.

Mwenyezi Mungu ailze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

Monday, 3 November 2014

show ya weusi ndani ya arushaaaaaaa jana cheki picha zote hapaaaaaaaaaaa....







Kwa zaidi ya miaka miwili wapenzi wa muziki jijini Arusha hawajashuhudia shangwe za Fiesta, lakini Jumamosi, November 1, Weusi walifanikiwa kuwapa show yenye ukubwa unaokaribiana na tamasha hilo la kila mwaka.
Wakiandaa wao wenyewe, Weusi walifanikisha kuvutia nyomi la kutosha kwenye uwanja wa Triple A jijini Arusha. “Mungu ametuonesha kwamba tunaweza kufanya makubwa zaidi ya vile tunavyofikiria,” Joh Makini ameiambia Bongo5.



Nyomiii
Joh amesema maandalizi makubwa wamefanya wao wenyewe japo wasambazaji wa kilevi cha K Vant waliingia kama wadhamini katika hatua za mwisho mwisho. Tamasha hilo Jumamosi hii linahamia mjini Moshi, La Liga, Nov. 15 watatumbuiza Mbeya, City Pub, Nov 22 ni Mwanza, Jembe ni Jembe halafu wanatarajia kumalizia Dar Nov 29.
Hizi ni baadhi ya picha za Arusha.