Sunday, 26 October 2014

naombeni ushauri juu ya mtasha huyu....






Ninae rafiki yangu mzungu wa Canada,huyu jamaa ananiambiaga nimtumie picha za watu walivyo maskini na nikiwa naongea nao,alituma pesa nikanunua Camera na laptop na huwa kila wiki ananitumia dola 50 nimemfanyia hii kazi kwa mwaka sasa na kuna wakati ananitumia hata dola 800 hata elfu moja ili niende mikoani.


Huyu mtu tulijuana kupitia biashara ya wadudu baadae akadai ameokoka kwamba ni mkristo na akaniuliza kwamba na mimi ni mkristo nikamwambia ndio amekuwa akiniuliza kuhusu bible na bible mimi siijui kwa undani sana japo ni mkristo na sijapata mda mzuri wa kujifunza.


Huyu mtu sijawahi kukutana nae face to face.Kusema kweli huyu mtu sijawahi kuumuulizaga madhumuni ya hizo picha japo yeye anadai anapenda kuwaona watu maskini kwenye picha ili awaombee.




Naombeni ushauri kwa watu wenye ujuzi zaidi na dunia.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment