Askari Polisi wawili wamejeruhiwa kwa risasi wakiwa katika mapambano na majambazi katika kijiji cha Nyakagwe mkoani Geita.ITV ilifika hospitalini na kuzuliwa kupiga picha kwa majeruhi hao mpaka uchunguzi utakapo kamilika ambapo kaimu kamanda mkoa wa Geita ACP Peter Kakamba amesema bado uchunguzi unaendelea na jeshi la Polisi litatoa ripoti baada ya taarifa kukamilika.
Akiongea na ITV kaimu mganga mkuu wa wilaya Dr George Mituhemela amesema wamepokea wagonjwa wawili ambapo mmoja amejeruhiwa katika mguu wa kulia na mwingine katika mkono wake wa kulia na mbavu katika upande wa kulia.
CHANZO:ITV
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
.jpg)
0 comments:
Post a Comment