Wednesday, 3 December 2014

SHEDDY CLEVER AFUNGUKA NA KUSEMA KWA NINI?,JINA LAKE ALIKUANDIKWA KWENYE VIDEO MPYA YA DIAMOND





Producer wa hits mbili za Diamond Platnumz ‘Number One’ na ‘Ntampata Wapi’ alionekana kufurahia mafanikio ya Diamond kwenye tuzo za Channel O, lakini kitu kimoja hakijakaa sawa moyoni mwake.



Sheddy amesema ameshangazwa baada ya kutoona jina lake likiandikwa kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’.

“Biashara kweli ni matangazo na nilitakiwa niandikwe kweli kwenye ile video, lakini sasa kwa sababu imeshapita na vitu vingi vimeshatokea na ukiangalia kwenye video international wanafanya hivyo ila mpaka sasa hivi najaribu kujiuliza sijapata jibu kamili kwanini wanafanya hivyo,” Sheddy ameiambia E-News ya EATV.
“Ukiangalia video za West Africa za akina Davido, Wizkid wengi producer wa audio wanakuwa hawaandikwi kwenye video. Sasa sijui wanafuta ule mfumo wa wenzetu, sifahamu.”

PICHA ZOTE MSANII>>>>>>> SHILOLE ALIVYOKINUKISHA UBELGIJI






Shishi Baby akifanya mambo yake huku mashabiki wakiwa na midadi.
Msanii Shilole akiburudika vyema na dada yetu aliyekuja toka Norway kujumuika nasi katika kupata burudani ya Shishi Beibii.

Wachaa weeee.

Msanii Shilole akipata kumbukumbu ya picha

Shilole akiwa na Balozi wa Madagasca nchini Belgium

Mapicha picha ya ukumbusho ya Shilole.

Dada Rose akiwa na Shilole.

Shilole aliombwa saini na balozi wa Madagasca[Mnyamwezi umetishaaaaa] wakakutangazeeee.

New artist Max at work.

Dili ikienda sawa Shilole kula donge nono,,,lini,wapi na saa ngapi Mungu ndio mjuzi,,,kaa mkao wa kula.

HUYU NDIYE SHABIKI NAMBAMOJA WA DIAMOND..ONA ALICHOKIFANYA


 



Ushabiki hauna mipaka kwenye mambo mengi ya burudani, michezo na hata siasa. Huyu anajiita shabiki namba moja wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz na kwa mapenzi ya ukweli jamaa amechora tattoo ya jina la msanii huyu kwenye kifua chake. Haijulikani kam ni tattoo ya muda mrefu au ya muda mfupi.

MAELFU WAFURIKA KUMZIKA PHILLIP HUGHES...!!!




Misa ya kumuombea mchezaji wa cricket wa Australia, Phillip Hughes ilifanyika siku ya jana katika nyumbani kwake jijini Macksville.


Waombolezaji wakiwa katika misa ya kuombea mwili wa marehemu, Phillip Hughes.

Kapteni wa timu ya taifa ya cricket ya wa Australia, Clarke akiongea jambo wakati wa misa hiyo.

Dada wa marehemu Megan akiongea jambo wakati wa misa.

Mwili wa marehemu ukiendelea kuombewa.

Wananchi wakifatilia misa kupitia Tv.

Mchezaji wa cricket wa Australia, Phillip Hughes enzi za uhai wake.

Safari ya kuelekea katika mazishi ikianza katika mtaa wa Macksville.

Wakisindikiza mwili wa marehemu, Phillip Hughes kwa kutembea kwa pamoja.

Wananchi wakiwa pembezoni mwa barabari kuaga mwili wa marehemu.

...Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari Macksville High School.

Mwili wa marehemu ukiwasili

Wananchi wakiendelea kuweka maua ndani ya uwanja wa cricket.

Wananchi wakiwa katika uwanja wa Cricket wa Sydney tiyari kwa kuaga mwili wa marehemu.

HAYA NDIYO MAAMUZI MAGUMU YA RAIS KENYATTA BAADA YA MAUAJI KUENDELEA NCHII KENYA




Baada ya nchi hiyo kuelemewa na mashambulizi mara kwa mara na shinikizo la wananchi Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi Waziri wa Usalama Joseph Ole Lenku na kumteua Waziri mpya wa Usalama Joseph Nkaiseri, kuchukua nafasi hiyo huku Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo akilazimishwa kuachia ngazi.
Baada ya lile shambulio la siku kumi zilizopita ambapo kundi la Al Shabaab liliwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri kwa basi kutoka Mjini Mandera karibu na mpaka wa Somalia, Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kujiuzulu kufuatia kukithiri kwa mashambulizi ya kigaidi na kuhatarisha usalama, ambapo jana Novemba 02 wachimba kokoto 36 wameuawa na kikundi cha Al Shaabab katika kaunti ya Mandera.


“… Hapa ni mahali tukemekaa kama mimi mwenyewe nimekaa miaka tisa ile mambo nashuhudia saa hii sijawahi jionea na macho yangu watu kuuliwa sijawahi ona, by the way maisha yetu iko hatarini…”


“...Nakimbilia usalama wangu juu nahofia pale kwa nyumba hujui watavamia lini watakuja lini, saa ndio natoka kwangu kwa nyumba nakaa nakuja kukaa hapa kulingana na ile mazingira tunayo nakaa hapa kupata ulinzi wa Serikali inakuwa ni ngumu sana, sisi ndio tunafanya msituni tulio eneo la hapa Mandera Town wavamivi wanavyokuja wanapita njia za misituni sasa Polisi kujua ni ngumu…”


Rais Kenyatta amesema kuwa baada ya mazungumzo na Kimaiyo alikubali kustaafu mapema kwa sababu zake binafsi.

Wagombea 68 CHADEMA Arumeru Mashariki wapingwa.



Wagombea 68 wa nafasi mbalimbali za uongozi katika jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamewekewa pingamizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutotimiza vigezo na masharti ya tume ya uchaguzi.


Baadhi ya wagombea hao waliowekewa pingamizi wa CHADEMA wametafsiri hali hiyo kama njama za kisiasa zinazofanywa na chama tawala kutaka kuwaathiri kisaikolojia na wamesema baadhi ya watendaji wa vijiji wanachangia kuwepo kwa hali hiyo.


Baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo mbunge wa jimbo hilo Mh Joshua Nassari wameziomba ngazi zinazohusika kushughulikia suala hilo kabla halijaleta madhara kwani kuendelea kulifumbia macho ni kutengeneza matatizo yasiyo ya lazima.


Akizungumzia malalamiko hayo katibu tawala wa wilaya ya Arumeru Bi Boma amesema wanaendelea kusimamia zoezi hilo kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya tume na kwamba wote wanahisi kuwa hawajatendewa haki, wana haki ya kukata rufaa.


Chanzo:EATV

MANCHETER UTD YAENDELEZA USHINDI, YAICHAPA STOKE CITY 2-1








MATCH FACTS

Manchester United (4-3-1-2): De Gea 7.5; Valencia 5.5, Smalling 6, Rojo 6.5, Young 6; Fellaini 7, Carrick 6, Herrera 7.5 (Fletcher 86); Mata 7 (Januzaj 90); Van Persie 5.5, Wilson 6 (Falcao 78)

Subs: Lindegaard, McNair, Blackett, Keane.

Goals: Fellaini 21, Mata 59.

Booked: Herrera, Young.

Stoke City (4-2-3-1): Begovic 6; Bardsley 5.5, Shawcross 6, Wilson 6, Pieters 5.5; Cameron 5.5, Nzonzi 7; Ireland 5.5 (Arnautovic 82), Krkic 7, Assaidi 5.5 (Crouch 77); Diouf 5.5

Subs: Butland, Muniesa, Palacios, Adam, Shenton.

Goal: Nzonzi 39.

Booked: Bardsley, Pieters, Ireland.

Man of the match: Ander Herrera.

Referee: Jon Moss 6.5.

Attendance: 75,388

Ratings by JOE BERNSTEIN at Old Trafford

PAUNDI MILIONI 50 KUMNG'OA EDSON CAVANI PSG WAKATI RADAMEL FALCAO AKIONESHWA MLANGO WA KUTOKEA MANCHESTER UNITED.






Imearifiwa kuwa klabu ya Manchester United inajiandaa kutuma ofa ya kiasi cha paundi milioni 50 kwenda kwa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa yenye lengo la kutaka kumng'oa mshambuliaji wa timu hiyo Edinson Cavani mara baada ya kuamua kutokumpa mkataba wa kudumu mshambuliaji Radamel Falcao.
Manchester United iko kwenye mipango ya kumsajili mshambuliaji anayekipiga kwa mkopo wa muda mrefu Radamel Falcao kutoka klabu ya Monaco kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 50,Lakini maumivu ya muda mrefu ya mshambuliaji huyo raia wa Colombia yanamfanya meneja wa klabu ya Man Utd Louis van Gaal kumtoa kwenye mipango yake.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinadai kuwa United inajiandaa kutuma ofa hiyo ili kumnasa huyo wa klabu ya PSG anayeonekana kutaka kukikimbia kivuli cha mshambuliaji mwenza wa timu hiyo Zlatani Ibrahimovich.

KAULI YA MSANII DIAMOND ESCAPE ONE,MARA BAADA YA KUPOKELEWA UWANJA WA NDEGE



Miongoni mwa vitu alivyovizungumza Diamond kwenye mkutano wake huu alisisitiza umoja kwa wasanii wa Tanzania ili kufikia nafasi ambazo nchi zingine kama Nigeria zimefika za kusimamisha wasanii wengi kwa pamoja.




Waandishi wa habari,mashabiki na wadau wa muziki jioni ya Dec 02 walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Diamond Platnumz ambaye ameingia mchana wa leo na kutoa nafasi hiyo jioni