Friday, 21 November 2014

Ni Diamond Platnumz kwenye XXL leo Novemba 21, isikilize hapa full interview…

 …
 

 
Kupitia millardayo.com siku ya juzi ulipata taarifa kuhusu nyimbo ya msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuachia nyimbo yake mpya ambapo kwa mara ya kwanza ilionyeshwa kupitia kituo cha MTV, na jana ikawa siku rasmi ambayo Diamond aliachia nyimbo hiyo.

Leo Novemba 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.

Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:

Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“

Diamond : “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“

Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play>>>>>>>>.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment