Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Watu wawili wameuawa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea mnamo tarehe 20/09/2014
majira ya saa 23:30hrs katika Kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani
Dodoma ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MWAJUMA D/O CHOMOLA
mwenye umri wa miaka 48, Mgogo mkazi wa Mzogole aliuawa kwa kupigwa na
Rungu tumboni upande wa kushoto na mume wake aliyefahamika kwa jina la
RICHARD S/O KODI mwenye umri wa miaka 55, Mhehe mkulima na mkazi
wa kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambaye nae
aliuawa tarehe 21/09/2014 majira ya saa 09:00hrs baada ya kushambuliwa
na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na alifariki dunia akiwa
anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa baada ya
wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo kafariki kutokana na
kipigo cha mume wake.
Kamanda
MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji
hayo ni wivu wa mapenzi kwani RICHARD aliuawa na wananchi baada ya
kumuua MWAJUMA ambaye alikuwa mkewake aliyekuwa akiishi nae, baada ya
kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo kijijini akidhani
kuwa ameenda kwenye masuala mengine.
Aidha Kamanda MISIME amesema wananchi waliojichukulia sheria mkononi bado wanatafutwa ili wafikishwe mahakamani.
ANKO SAM BLOG
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment