Thursday, 9 October 2014

WALIOMFANYIA UNYAMA MWANAUME MWENZAO WAPANDISHWA KIZIMBANI

 
WASHITAKIWA wanaokabiliwa na mashitaka ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii, wamepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali ambapo walidaiwa kumlawiti mwanaume mwenzao na kumpiga picha kwa madai ya kutaka kulipwa Sh milioni moja.
 
Washitakiwa hao ni Erick Kasira (39) na Juma Richard (31) ambao wanadaiwa kulawiti sanjari na kupiga picha za tukio hilo.
 
Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Said Mkasiwa kwamba Agosti 23 mwaka huu, maeneo ya Maembe Bar & Guest House, iliyopo Kiwalani Yombo walimkuta Kambi akiwa na Sanifa Bakari katika chumba namba sita ambapo walimshutumu kuwa wana mahusiano baada ya mshitakiwa mmoja kudai kwamba ni mke wake na kwamba wamemfumania.
 
Washitakiwa hao walimtaka Kambi kutoa kila alichonacho na kuwakabidhi kompyuta aina ya HP yenye thamani ya Sh 350,000, fedha taslimu Sh 100,000, simu aina ya Tecno yenye thamani ya Sh 350,000 na viatu.
 
Walidaiwa baada ya kumkuta Kambi akiwa na Sanifa kwa madai ya kwamba wana mahusiano, walimlawiti kinyume na maumbile kisha walimpiga picha huku wakiwa uchi.
                ANKO SAM BLOG

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment