Tuesday, 28 October 2014

MSANII YOUNG DEE AKANA MADAI YA KUKACHA SHULE




Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Young Dee akiwa katika studio za Global TV online.
makala: Chande Abdallah
Leo hii kwenye Live Chumba cha Habari ya Global Publishers tunaye bwa’ mdogo machachari anayewakilisha vilivyo kwenye muziki wa Hip Hop, Young Dee. Dogo anafanya poa na nyimbo zake kadhaa kama: Dada Anaolewa, Tunapeta, Fununu na Siyo Mchoyo.
Katika mahojiano na safu hii inayorushwa
pia kupitia Global Tv Online, Young Dee anafunguka kuwa alikuwa akiupenda Muziki wa Hip Hop kiasi cha kuvizia mama yake ambaye ni msikilizaji mzuri wa muziki wa Injili, akiwa ameenda kazini ndipo asikilize muziki huo.


Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo kwa kirefu zaidi yanapatikana kupitia tovuti ya
Mwandishi: Ulianzaje muziki?
Host wa kipindi cha Mtu Kati cha Global TV, Pamela Daffa (kushoto) akijiandaa kufanya mahojiano na Young Dee.
Young Dee: Ilitokea tu kwamba kila mtu aliyekuwa akinizunguka alikuwa akisikiliza muziki wa aina moja tu ambao ni Hip Hop pekee hivyo na mimi nikatokea kuupenda sana.
Mwandishi: Inasemekana uliacha shule kwa ajili ya muziki, kuna ukweli wowote hapo?
Young Dee: Hapana sijawahi kuacha shule. Nimesoma hadi O- level, nikamaliza form four sema kuna mambo ya kifamilia ambayo sitaweza kuyaongelea hapa ndiyo yaliyonifanya nisiweze kuendelea tena.
Mwandishi: Kwa nini unajiita Young Dee wakati wewe ni mkubwa siku hizi je, umefikiria kubadili jina lako baadaye?
Young Dee: Ahhaa! Kwanza mimi bado mdogo, nina miaka 22, bado nipo Young na ningependa baadaye nijiite ‘Forever Young’ kama a.k.a yangu mpya na hata kama nikiwa mkubwa bado akili yangu ni kama kijana kwa hiyo jina la ‘Young’ litaendelea.
Mwandishi: Nini ukikifanya utajiona umefanikiwa zaidi?
Young Dee: Nataka kufikia levo kwamba vijana waniangalie mimi kama mfano kwao katika kufanikisha malengo yao kupitia mimi. Nikifikia hatua hiyo, hapo nitajiona nimefanikiwa sana.
Pamela Daffa (kushoto) akipozi na Young Dee.
Waandishi: Inasemekana kuwa wasanii mliotoka kwenye gemu mnaringa sana kwa wasanii wadogo pindi wanapotaka kolabo na nyinyi, hilo unalizungumziaje?
Young Dee: Mimi siringi ila nina complications kwenye kolabo kwa sababu mimi ni bidhaa hivyo lazima niangalie nitanufaika vipi na hiyo kolabo, siwezi kufanya kolabo na kila msanii, wengine hawana uwezo kabisa wa kuimba ila wanataka kolabo, kuna wengine wana uwezo kiasi kwamba inafikia hatua hata nauli najitolea na kufanya nao kolabo bure kabisa.
Mwandishi: Nini ambacho unatarajia kufanya kwa ajili ya mashabiki wako?
Young Dee: Nina albamu ambayo ipo njiani pia nina ‘reality show’ ambayo itakuwa maalumu kwa mashabiki wangu wa ukweli kabisa.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment