Ndugu jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika kifo
baada ya ajali ya mtumbwi kutokea katika kijiji cha kalalangabo wakiwa
wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma
Bibi harusi Mariamu mduwa aliyenusurika kifo katika ajali ya mitumbwi
katika kijiji cha kalalangabo akiwa naendelea na matibabu katika
hospital ya mkoa wa Kigoma
Waokoaji mbalimbali wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya
mitumbwi iliyobeba harusi kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha
Kigalya kutafuta miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana
WATU sita wamekufa maji katika ziwa Tanganyika na wengine kumi na moja kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi Mariamu Mduwa baada ya mitumbwi miwili waliyo kuwa wakisafiria kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji Kigalye kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika kuzama ziwani.
Tukio hilo limetokea leo saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo kupigwa wimbi kali na kuzama katika kijiji cha Kalalangabo wakati bwana harusi huyo akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani akiwa na ndugu na jamaa pamoja na wapambe.
Akiongea na mtandao huu katika wodu namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
”Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo,kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia mungu”alisema bibi harusi huyo
Muhanga mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
”Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika kungekuwa na barabara tungepita barabrani”alisema Mhanga huyo
Naye muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa wamejuhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na mpaka sasa wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa,na miili sita kuopolewa pamoja na walionusurika 11,lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi ambao bado haijapatikana kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya sabini.
ANKO SAM BLOG
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:
Post a Comment