
Shughuli
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta zilisitishwa kwa
muda Jumatano asubuhi baada ya mwili wa kijana mdogo kupatikana karibu
na eneo la kurukia ndege
Mkuu wa
kitengo cha Polisi katika uwanja huo, kamanda, Joseph ole Tito, amesema
kuwa mwili huo ulipatikana katika sehemu ya kurukia ndege
Hata hivyo alisisitiza kuwa ndege zilizokuwa zinaingia uwanjani humo asubuhi na mapema hazikuathiriwa na tukio hilo.
Halmashauri ya huduma za ndege ilisema kuwa uwanja ulifungwa kwa dakika arobaini baada ya maafisa wa usalama kugundua mwili huo.
Kwa mujibu wa maafisa hao, hatua ya kufunga uwanja huo ilifanywa ili kuondoa mwili wa kijana huyo.
Ni ndege
ya shirika la ndege la Uturuki tu ndiyo ililazimika kusalia angani kwa
muda huku mwili wa kijana huyo ukiondolewa uwanjani.
Kijana huyo anaaminika kuwa na kati ya umri wa miaka 10 na 12 na alikuwa na majeraha upande wa kushoto wa mwili wake.
''Mwili wake uliondolewa katika eneo hilo na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa,'' alisema bwana Tito.
Polisi
wamesema watafanya uchunguzi kubaini ikiwa alianguka kutoka kwa gurudumu
la ndege au mtoto huyo alifariki kutokana na sababu nyinginezo.
Pia miongoni mwa maswali yanayoulizwa ni vipi mwili wake ulipatikana katika uwanja wa ndege hasa katika njia ya kurukia ndege?
Visa vya
watu kupanda kwenye magurudumu ya ndege kimagendo kwa lengo la kusafiri
kwenda nchi nyingine vimekuwa vikiripotiwa hivi karibuni.
CHANZO BBC.Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment