
Waziri Samuel Sitta akizungumza baada ya kupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo akisoma taarifa ya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Baraza la Mawaziri. Wengine kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera, Waziri Mh. Samuel Sitta na Mwandishi wa Taarifa za Mkutano Mpya kutoka Uganda Bi. Mary Nankabirwa.

Mwenyekiti anayemaliza muda wake Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi. Phyllis Kandie (katikati) kabla ya kukabidhi uenyekiti kwa Waziri Samuel Sitta wa Tanzania. Kushoto ni Bw. Mugisha Kyamani kutoka Tanzania ambaye alikua ni Mwandishi wa Taarifa za Mikutano kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita

Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).

Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Miundombinu Dkt. Enos Bukuku walipokutana Jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki. Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment