AZIDI KUKERWA
Ngoja niseme ukweli kwamba kwa maneno ambayo alikuwa akiyazungumza siku hiyo yalinichefua, yakanifanya nizidi kuwachukia wasichana ambao kwa jinsi nilivyokuwa, nilitegemea ningepata sapoti kubwa kutoka kwao lakini wao ndiyo walikuwa wa kwanza kunikandamiza.
Ila sipendi urafiki wangu na wasichana wenzangu, niliwaambia baadhi ya wavulana, walikuwa miongoni mwa marafiki zangu.Kwa nini?îìTuna fitina sana, unajua mimi kama msichana ninapofanya kitu huwa ninahitaji kupewa sapoti kwa kile ninachokifanya. Ulimsikia Fatuma alivyosema?î
ìHapana, alisemaje?î
ìAmenikera sana.î
ìAmefanyaje?î
ìWewe jua tu amenikera.î
ìSasa ndiyo hautaki kuniambia amekukeraje?î
ìNinataka kuimba, kuwa mwanamuziki.î
ìHilo tunafahamu. Sasa kuna tatizo?î
ìNinahitaji kuungwa mkono, ninahitaji niendelee kuimba na kupongezwa,î niliwaambia wavulana hao.
ìHilo si tatizo, sisi si tupo hapa kukupa kampani?î
ìNdiyo, ila Fatuma kanikera. Eti nina sauti mbaya! Kama yeye anajua kuimba si angeimba! Tatizo lipo wapi sasa?î niliuliza.Kiukweli nilikasirika, chuki yangu juu ya wasichana iliendelea kuongezeka. Sijui kama walikuwa wakiambiana au la, kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo walijitokeza wasichana wengi na kuchukia kwa kile nilichokuwa nikikifanya.
Kama mwanadamu, kuna kipindi nilikata tamaa, kuna kipindi nilikaa chini na kuhuzunika, kuna kipindi nilinyongíonyea lakini baada ya muda, kuna nyakati zikafika ambazo nilitiwa moyo na kidogo kuendelea kusonga mbele.
Mpaka leo hii nimefikia hapa nilipo, sikufika kiwepesiwepesi, kuna waliokuwa wakinitia moyo na kunivunja moyo, walikuwepo wale ambao hawakupenda kuniona nikifika hapa nilipokuwa, pamoja na hayo, niliendelea kwenda mbele. Mwaka ukakatika na kuingia kidato cha pili, hakukuwa na uafadhali hata kidogo.
****
AANZA KUIMBA NA KUNDI
Miaka iliendelea kukatika mpaka nilipomaliza kidato cha nne na ndipo nikakaa nyumbani kusubiri matokeo. Katika kipindi chote hicho nilikuwa na shauku kubwa ya kuimba hivyo niliendelea kujitungia nyimbo zangu zenye maadhi ya taarabu na kujiimbia chumbani kwangu.
Baada ya matokeo kutoka na kutokufikisha alama ambazo nilitakiwa kufikisha, nikaamua kuingia moja kwa moja kwenye muziki kwani sikutaka kuolewa mapema kama walivyokuwa wakifanya wasichana wa umri wangu ambao waliona ndoa kuwa kila kitu.
Nikajipanga na kuanza kucharakia maisha yangu katika uimbaji kitu ambacho baadae nikafanikiwa kujiunga na kundi moja liitwalo Culture Music All Club.ìKama anajua kuimba, mpenzi nafasi, hakuna kumbania mtu,î alisema kiongozi wa kundi hilo siku ambayo nilikwenda kujiunga nao, na mimi nilitaka kuwa mmoja wa kundi hilo.
ìTunataka kutikisa Tanzania nzima, utaweza kuipeperusha bendera ya Zanzibar kupitia muziki?î aliniuliza msichana mmoja, simkumbuki jina lake, ila alikuwa miongoni mwa watu wenye busara ambao nimewahi kukutana nao katika maisha yangu.
ìNitaweza tu, ondoa shaka,î nilimjibu huku nikijiamini.
SIku hiyo nilikaribishwa rasmi na kuanza kuimba ndani ya kundi hilo. Kiukweli, mara nilipoanza kuimba tu, kila mtu alivutiwa na sauti yangu, ilikuwa ikisikika vizuri tofauti na baadhi ya watu niliowakuta mahali hapo.
Kila mmoja akaanza kuisifia, sikuwa mtu wa majivuno, kila aliyekuja na kunisifia kwamba nilikuwa na sauti nzuri, nilimwambia shukrani zote ziende kwa Mungu kwani yeye ndiye aliyenipa sauti hii.Niliendelea kuimba ndani ya kundi hilo, mara nyingi tulikuwa tukitwa katika sherehe mbalimbali za viongozi na wakati mwingine kuanziasha matamasha yetu wenyewe ambapo watu waliingia kwa viingilio na kupata burudani.
Sifa za sauti yangu hazikuishia hapo, hata watu waliokuja kuingia katika matamasha mbalimbali ambapo kundi letu lilikuwa likitumbuiza, nilikuwa nikisifiwa sana, taratibu nikaanza kuwa maarufu, hiyo ilikuwa mwaka 1991. Kitambo sana ila bado nakumbuka mengi.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment