Thursday, 27 November 2014

HIZI NI TETESI NZITO KWA SIKU YA LEO, BAADHI YA WABUNGE WA WADAIWA CCM WAHONGWA MILION 3 ILI KUTETEA WATUHUMIWA WA UFISADI






· BUNGE LA TANZANIA


Zipo tetesi kuwa Wabunge wa ccm kila mchangiaji atahongwa milioni 3.
Hapa Dodoma kumezagaa taarifa kuwa wabunge wote wa ccm waliochangia jana na watakaochangia leo wamehongwa fedha taslimu milioni tatu ambapo inadaiwa kuwa genge la mafisadi hawa limejichimbia katika hoteli moja mjini hapa kuhakikisha wabunge wa chama tawala hasa wale vichwa pasi wanatulizwa na kugeuzwa muono wao juu ya escrow ili watete Pinda na wenzie wasijiuzuru na kuwajibishwa.
Taarifa zinabainisha kuwa genge hilo linaratibiwa kwa ushirika wa ofisi ua spika ambapo ofisi hiyo ilitoa orodha ya wachangiaji wa leo wa ccm nq baada ya kumaliza tu mda huu wamekwenda kila mmoja na njia yake kwenda kuchukua fedha hiyo.
"Jamaa wapo Dodoma hotel na saint Gasper, ukiwatetea unavuta"
Sehemu ya maneno ya mheshimiwa Mbunge wa Ccm. Tayari TAKUKURU na Idara zingine za usalama wanafuatilia tukio hili kwa ukaribu

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment