![](https://fbcdn-sphotos-d-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xfp1/v/t1.0-9/10606585_317122001806828_6772117903715700802_n.jpg?oh=8a982af1190bcef7453610395c2c782c&oe=54C27DDB&__gda__=1422513234_16a0013488ae4497d5535f5bdf3d54eb)
SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 2
Mtunzi; Timotheo Mathias
Simu yake-0765676242
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa.
Sehemu ya 1 ilipoishia..........
Nilikuja
kuzinduka nikiwa na makovu mwili mzima na kutazama pembeni yangu
nilikuta joka kubwa likiwa na vichwa vinne na kila kichwa kilikuwa na
mapembe mawili.
Endelea...............
Kulingana na uchovu
niliokuwa nao sikuweza kufanya chochote nilibaki nikishangaa nikiwa sina
hata nguvu za kuweza kuinuka na kukimbia.
Ghafla
alitokea babu ambaye alikuwa mnene sana akiwa mkononi ameshikilia
kibuyu sikujua cha nini, alisogea mpaka nilipokaa ,aliponisogelea
niliweza kushuhudia kwa macho yangu joka likigeuka na kuwa pete nyeupe.
Babu aliisogelea ile pete na kutamka maneno ambayo sikuweza kuyafahamu baadaye na kuichukua ile pete.
Nikiwa nimekaa babu aliniamrisha niinuke, nilishangaa sana maana sikuweza kujua nguvu nimepata wapi?.
Babu
alininyoshea kidole chake cha kulia na kusema "kijana mwisho wa maisha
yako ulikuwa umefika lakini kulingana na nyota yako nzuri ndiYo maana ni
mzima na upo hapa nishukuru mimi maana waliokupeleka walikuacha peke
yako.
Sasa
basi kuanzia sasa utakuwa bega kwa bega na mimi, nitakusaidia
,nitahakikisha unarudi uraiani kwa wazazi wako, ukaendelee na masomo
yako.
Chukua hii pete usijaribu kuitupa hata kuvulishwa na mtu wa aina yoyote".
Nikiwa
nimesimama babu alipotea ghafla na baada ya muda mfupi ,yule mama
niliyekuwa naye hospitali ,alikuja .lakini alipofika karibu yangu na
kuiona pete niliyopewa aliitazama kisha akafyonza kwa dharau.
Sikujua anamaanisha nini.
Alinishika
mkono na kuniamuru nifumbe macho,baada ya kama sekunde 30 aliniambia
nifumbue, sikuweza kutambua maeneo tuliyofikia, kulikuwa na nyumba moja.
Mama
aliniambia nimfuate kwa nyuma mpaka mlangoni mwa nyumba tuliyofikia,
tulipokaribia tulisimama kwa muda mfupi, baadaye mama mwingine alitua
sehemu tuliyokuwepo.
Wakasalimiana, wote wakafurahi, sikujua kipi kilichotupeleka kwenye híi nyumba tena usiku!.
Mama
tuliyekuja naye alinisogelea na kuniambia tunaingia humu ndani kuchukua
watu wakatusaidie kulima usiku wa leo baadae watarudi, nikamjibu sawa.
Tukiwa watatu kwa pamoja tulisogea karibu na mlango,yule mama tuliyekuja naye alisema tukae pembeni aweze kufungua mlango.
Alisogea
karibu na mlango, aliposogea aliushika mlango pande zote nne akarudi
kama hatua mbili nyuma, akageuka na kuvua sketi yake akainama.
Mlango
ulianza kufunguka taratibu bila mtu yeyote kujua na alipohakikisha
umefunguka aliinuka na kuvuta sketi yake na kutuita kwa ishara ya mkono
kwa pamoja.
Wote
tuliingia ndani ya nyumba tukapitiliza hadi chumbani ,tulipofika
tulikuta watu watatu wamelala kitandani ,sikujua ni jinsia gani?
Mama
alisogea kwenye kona ya chumba akasimama na kunyosha mkono wake sehemu
ya kitanda, niliona mtu mmoja wa kiume (pande la jamaa) akiinuka
taratibu na kuufuata mkono wa mama ulipo.
Alipofika
alimshika mkono na kutoka naye nje ya nyumba, tulipofika nje
,alinikabidhi na kuniambia nimpeleke akalime nikiambatana mama aliyekuja
peke yake atanitangulia mbele yangu nikiwa mimi nimebebwa mgongoni na
jamaa tuliyemchukua.
Tukiendelea
na safari ya kwenda shambani ghafla nilikia kishindo kikubwa pembeni
yangu nikatazama na kuona likitokea vumbi likiambatana na kimbunga,
upepo mkali ulivuma hadi tulipo na kumshuudia mama aliyekuwa akiniongoza
njia akianguka chini na kuanza kutoa mapovu mdomoni hatimaye aliaga
dunia.
Nilibaki
nikishangaa mithili ya barafu kwenye friji, nikiwa natafakari, ghafla
Babu alinitokea mbele yangu akiwa anahema kwa nguvu na kwa kutisha mpaka
nilimuogopa.
Alinyanyua mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia mkia wa ng'ombe na kunisonta kidole akisema "nimekupa
pete ili uweze kujiokoa na kuwaokoa walio hatarini lakin leo hii
umeanza kuwatumikisha watu wasio na hatia!!!!?? Unabebwa mgongoni unaona
raaaahaaaaa!!!? Pumbavuuuuuu!!!!? mkubwa shuka mgongoni? na umurudishe
kwake fanya haraka?".
Kabla
sijashuka Babu alipotea ghafla, baada ya muda mama niliyemuacha nyuma
alikuja na kuniangalia kwa kunipandisha na kunishuka, akaniuliuza
mwenzako yuko wapi?
Niligeuka
ili niweze kumuonyesha alipoangukia na kufa lakini nilishangaa
kutokuuona mwili wake wakati amekufa muda si mrefu!, nilibaki
nikishangaa mwili umeenda wapi? Lakin sikupata jibu.
Mama
aliniamuru nifumbe macho baada muda nikafumbua, nilikuwa sehemu ya
kambi nikiwa na misukule wenzangu walioonekana kunishangaa sana mpaka
viongozi wa wachawi hasa pete niliyokuwa nimevaa kwenye kidole changu.
Tukiwa
tumepumzika, misukule kulingana na kwamba hakuna muda wa kunyoa nywele
zilirefuka kupita kiasi, wengine wakijaribu kukumbushia michezo
waliokuwa wakiipenda enzi za uhai wao, pia wengine walikuwa wakisukana
lakini mimi nilikaa pembeni na Sheila tukiwa tunabadilishana mawazo.
Baada ya muda msukule mmoja alitumwa kunifuata nilipokuwa nimekaa na kuniambia ninaitwa na mkuu wa wachawi.
Niliinuka na kuelekea sehemu alipokuwa amekaa nilipofika aliniangalia sana hasa sehemu ya pete ilipokuwa.
Alipomaliza alitabasamu na kusema "Kijana
naona sasa umekuwa na unajiona sana mpaka inafikia mahala unaua watu
wangu!!!? Sasa basi kulingana na ushenzi ulionifanyia nakupa kazi ya
kunitengezea mafuta lita 5 ya mtoto mchanga utasaidiana na watu wangu
nitakaokupa, kazi hiyo kufikia kesho uwe umeshamaliza",aliniagiza mkuu
wa wachawi.
Niliondoka
na kuelekea sehemu niliyokuwa nimekaa na Sheila, nikiwa natafakari
mtihani niliopewa Sheila aliniuliza vipi kuna tatizo?
Nilimjibu ndiyo kuna tatizo, nimeambiwa nitengeneze mafuta lita 5 ya mtoto mchanga.
Sheila alisema mbona hapa gambosi kitu cha kawaida sana maana tunaishi kwa mafuta ya watoto wachanga.
Nilimuuliza
kivipi? Sheila alisema mtoto mchanga hasa yule hajatimiza miezi tisa
akiwa tumboni mwa mama yake huchukuliwa na kupikwa maana viungo vyake
bado vilaini huyeyuka na kuwa mafuta.
Mafuta hayo huchukuliwa, na hayo mafuta hutumika kwa kupaka sehemu za macho na binadamu wa kawaida hawakuoni.
Nilimuuliza je, watoto hao wachanga hutoka wapi?
Sheila
alinijibu hutoka kwa mama viongozi wa wachawi kila baada ya miaka 10
kila mama anatoa mtoto, pia wengine huchukuliwa kwenye hospitali kwa
miujiza pindi wanapomaliza kuzaliwa tu!.
Tukiwa
kwenye mazungumzo na Sheila ,mama mmoja alikuja kunichukua na kwenda
sehemu husika ya kupikia watoto, nilikuta moto mkali ukiwaka huku juu
yake kuna sufuria lililo chemka mpaka linakuwa jekundu.
Mama
huyo aliniletea kitoto kichanga kikiwa hai na kuniamuru nikitupie ndani
ya sufuria harafu nianze kukaanga mpaka nihakikishe yamekuwa mafuta
ndani ya sufuria.
ITAENDELEA JUMAMOSI IJAYO KUPITIA www.mbelwasamwel.blogspot.com
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment