Sunday, 26 October 2014

HATARI....POLISI YAKAMATA MABOMU MANNE YA KIVITA HUKO ZANZIBAR



Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamtwa kwa mtu huyo ambaye kwa Mujibu wa jeshi hilo mtu huyo amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa kuagiza, kuingiza na kuhifadhi mabomu ya kivita ya kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani huku kamishna akidai mtandao huo unausishwa na matukio kadhaa.



Hata hivyo kamishna Hamdani Maka amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye hata hivyo amekataa kumtaja jina na mazingira ya ukamataji wake amesema hausiani na imani ya kidini na polisi inamshughulikia mtu kisheria kutokana na kosa lake kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo Imani za kidini.


Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yeyote kuhusu mtuhumiwa huyo jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu akipelekwa nje ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema bado polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la Zanzibar au la, ama ni mtandao wa ugaidi wa nchi nzima

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment