![](https://scontent-a-vie.xx.fbcdn.net/hphotos-xpa1/v/t1.0-9/s480x480/10625040_501812816622852_3835715223623918998_n.jpg?oh=ba04aff81b78331a1782b899606d37c0&oe=54C16053)
Harusi
ya Eric Holder, 45, na aliyekuwa mama yake wa kambo Elisabeth Lorentz,
48, ilifanyika katika kijiji cha Dabo, karibu na mji wa Metz.
Imeripotiwa kuwa mume wa zamani wa bi harusi, ambaye ni baba wa Bwana Holder, alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Sheria za Ufaransa zinapiga marufuku ndoa kati ya watoto wa kambo na wazazi wa kambo, lakini mahakama ilitoa uamuzi wa ndoa hiyo kufanyika.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilipinga uamuzi huo wa mahakama katika eneo la Lorraine, lakini ikaamua kutokata rufaa.
Awali,
wawili hao walipeleka malalamiko yao hadi katika ofisi ya Rais Francois
Hollande - lakini walipata barua kuthibitisha kuwa ndoa za aina hiyo ni
marufuku.
Baada ya uamuzi wa mahakama, bi harusi alisema: "Hatimaye, ile siku kuu imewadia!"
"Kwa
kweli nina imani kuwa habari yetu itasaidia wapenzi wengine waliopo
kwenye hali kama hii, kwa sababu najua wapo kadhaa," ameliambia shirika
la habari la AFP.
Bi harusi huyo ameongeza kusema kuwa mume wake wa zamani amekuwa "akiwaunga mkono" katika mapambano ya kisheria.
ANKO SAM BLOG.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment