Katika hali isio ya
kawaida huko maeneo ya bahari ya Shamiani (kwa gombe) jimbo la kiwani
mkoa wa kusini Pemba kumeibuka kiumbe kikubwa cha ajabu kutoka baharini
ambacho kimepwewa. Kwa mujibu wa taarifa toka kwa baadhi wakaazi wa
maeno ya jirani na eneo hilo ambao wamefurika kwa wingi kwenda kuona
kiumbe hicho wamesema kuwa ni mara
ya kwanza kuona kiumbe cha namna hio kikiwa kimepwewa ndani ya bahari.
Baadhi yao wameleza kuwa huenda pengine kiumbe hicho cha ajabu chenye
urefu takribani mita 40 na upana zaidi ya mita 25 kikawa ni samaki aina
ya nyangumi au chongowe. Katika hali ya kushangaza ndani ya fukwe hizo
za bahari ya kwa gombe watu zaidi ya 200 kutoka maeneo jirani ya likoni,
mwambe na ngambu shamiani wamejitokeza kuona kiumbe hicho cha ajabu
ambacho tayari kimekufa. Aidha makundi ya wananchi wanaendelea kukata
minofu ya aina hio ya kiumbe huku wengine wakijaza madumu yao mafuta
yanayotiririka kutoka kwa kiumbe hicho. Kwa upande wake mtalamu wa
viumbe vya bahari Zanzibar kwa masharti ya kutokutajwa jina amesema
msimu huu viumbe vya bahari aina ya nyangumi hupita katika ukanda wa
bahari ya hindi. ‘’Inaonekana baadhi ya watu huwapiga aina hii ya viumbe
vya bahari ndio maana hufariki dunia,hali hii inaitia nchi yetu jina
baya kimataifa kuonekana tunawauwa kwa makusudi’’aliongezea mtaalamu
huyo. Alieleza kuwa kitengo chao kimeshatoa elimu sana ili wananchi
waache tabia hii ya kuwangamiza viumbe hawa kwani dunia haikubali kwa
sasa kwa vile ni viumbe adimu na muhimu. Aidha alieleza jumuaya
(Skubado) inaweza kutubana kwa jambo hili na ameshauri wananchi
ikitokezea wamemuona kiumbe aina hii kipo hai basi watoe taarifa kwa
wahusika ili aweze kurudishwa baharini. Hali hii ya kuonekana kiumbe cha
ajabu ni mara ya kwanza kwa maeneo haya ambapo kumeibua mshangao
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment