Na Daniel Makaka, Sengerema
NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya
moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha
Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani
Sengerema mkoa wa Mwanza.
Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia
tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote
vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa
kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.
Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba
aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo
vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo
la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado
inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.
…..Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.
Awali Katibu wa kamati ya maafa
wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio
hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo
Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na
chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la
pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la
kanisa Katoliki kisiwani humo.
Pia alisema kati ya wahanga hao
hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zlizokuwemo
kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku
zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika
kisiwa hicho.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment