
Akizungumzia
hali hiyo juzi mbele ya waandishi wa habari, Naibu Kadhi Mkuu wa
Zanzibar, Hassan Othman Ngwali, alisema kwa sasa peke yake kuna kesi
1,917 za talaka mbele ya Mahakama sita za Unguja.(MM)
Mbali na
kuwa na kesi hizo, Ngwali alisema wanawake wamekuwa waathirika wakuu
baada ya kuvunjika kwa ndoa, kwa kuwa hakuna hukumu ya kesi zilizopita,
ambayo haki ya mgawanyo wa mali kwa wanandoa imetolewa.
Alitaja
baadhi ya sababu zinazochangia kuwepo kwa wingi wa talaka Zanzibar, kuwa
ni pamoja na wanandoa wenyewe kukosa mafunzo ya ndoa na majukumu yake
kwa ujumla.
“Moja ya
tatizo la kuvunjika kwa ndoa katika jamii, ni wanandoa kukosa elimu
ambayo itawafanya kujua haki na faida zinazopatikana katika ndoa,”
alisema.
Alisema
Ofisi ya Mahakama ya Kadhi imeanza kutoa elimu kwa makadhi wote kuhusu
haki za wanandoa katika kipindi chote wanapokuwa kwenye ndoa.
Naye
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Bakari Mshibe,
alisema marekebisho ya Sheria ya Mahakama ya Kadhi, yapo katika hatua za
mwisho kuwasilishwa mbele ya Baraza la Wawakilishi.
Alitaja
baadhi ya mambo yaliyofanyiwa marekebisho kwa lengo la kuimarisha
Mahakama hizo, kuwa ni pamoja na kutoa uwezo wa kumshurutisha mwanamume
kutoa matunzo ya mtoto wakati ndoa inapovunjika.
“Moja ya
mambo yaliyopewa kipaumbele katika marekebisho ya Sheria ya Mahakama ya
Kadhi, ni kuwabana wazazi ambao hawatoi matunzo kwa watoto wakati ndoa
inapovunjika,” alisema.
Wanaharakati
wengi Zanzibar, wanataka kuwepo kwa marekebisho makubwa katika Sheria
hiyo ya Mahakama ya Kadhi, hasa katika mgawanyo wa mali kwa wanandoa
wakati wanapotengana
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment