Tuesday, 19 August 2014

Maajabu ya dunia-KUTANA NA JIWE LA AJABU,LIMEOTA CHUMA JUU YAKE,LIKO TUKUYU MBEYA


Jiwe hili lipo katika kata ya ilima, nje kidogo ya mji wa Tukuyu Mbeya katika barabara ielekeayo Kyela, ni jiwe ambalo juu yake kuna chuma ambacho hakijafungwa kwa nati wala kitu chochote lakini hakitikisiki wala hakitoki.

 Inasemekana jiwe hili liliwekwa enzi za ukoloni na koloni la mwingereza.

 Miaka kadhaa iliyopita wananchi wa eneo hili walitaka kujua chini ya jiwe kuna nini? ndipo walipoamua kuchimba ili kujua kuna nini lakini hawakukuta kitu chochote.

Baada ya kukuta hakuna kitu chochote ndipo walipotaka kuliangusha ili lisiwepo kabisa walijaribu kutaka kuliangusha pasipo mafanikio kwa sababu halikuonesha mwisho wake ni wapi kwa kwenda chini.
BY ANKO SAM

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment