Hekima huja sio tu kwa
kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua
katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo tayari kusikiliza sauti
mhimu toka moyoni mwako.Miongoni mwa sauti hizi ni pamoja na ile nia
ya kutafuta ukweli wa jambo, kutafta maamuzi sahihi na kupata mawazo
endelevu , na yakinifu. Endapo mmoja ana kiu katika kuona matunda ya
sauti hizi, huyu mtu ni wazi kuwa ana chemichemi za hekima ndani yake.
Kama ilivyo kwa ufahamu, hekima halikadharika hupatikana kwa mtu yeyote
aliye na nia kama zilizotajwa hapo juu. Huyu mtu wa hekima na busara
hutoka katika tabaka la aina yeyote.Kuanzia kwa wazee, vijana, wanaume,
wanawake, mabwana, watumwa, tajiri,
masikini, wasomi hadi wasiosoma .Matabaka haya ya watu katika jamii
hayahukumu mgawanyo wa hekima na busara ndani ya vichwa vya
wanajamii.Hugawanya tu mitazamo yao. Kutokana na hali hii tunapata
misemo, maneno, nahau na methati juu ya maisha, kazi, dini , tamaduni na
vitu chungumzima vinavyosukuma gurudumu la jitihada katika maendeleo
ndani na nje ya jamii zetu . Misemo, maneno na aina nyingi za fasihi
simulizi mara nyingi zimekuwa haziathiriwi na vipindi, nyakati hata
muda. Ni kwa kuwa fikira pevu,chanya na yakinifu zilitumika kuchimbua
mizizi ya hekima iliyokuwa imejificha chini sana. Na hizi fikira ni
matokeo ya ugumu na urahisi wa mapambano ya kila siku zidi
ya maisha , yanaoibua uzoefu wa kukabiliana na changamoto za mara kwa
mara au zile zinazofanana. Hapa ni maneno na misemo ya maisha toka kwa
watu kumi mashuhuri duniani.
1.''Maisha ni kile kinachokutatiza wakati unapangilia mikakati yako ''John Lennon(mwanamziki)2.''Maisha ni asilimia 10 ya kile kinachonipata na asilimia 90 ni kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali'' Charles Swindolls(mchungaji)
3.''Muda wako unakikomo, kamwe usipote kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu mwingine''Steve Job(mhasisi wa Kampuni ya Apple )
4.''Maisha huchanua na kusinyaa kutokana na ujarisi wa mtu husika''Anais Nin(mwandishi wa kihispania)
5.''Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotaraji''Henry David Thoreau(mwandishi wa kimarekani)
6.''Maisha hayapimwi kwa idadi ya pumzi tuivutayo ,hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu''Maya Angelou(mshairi)
7.''Changamoto hupendezesha maisha,na kukabiliana nazo ndio maana halisi ya maisha''Joshua J Marine(mtoa nukuu)
8.''Mtu hata badili maisha yake kama hakuanza na kubadiri fikira zake''William James(mwanasaikolojia)
9.''Kwa kutazama tu ulichonacho maishani ,kila siku utahisi unazaidi,ila kwa kutazama unachokosa maishani kamwe hutokuwa na zaidi''Oprah Winfrey(muongozaji wa maonyesho ya televisheni)
10.''Maisha ni kile ukitendacho,ipo hivyo.itakuwa hivyo''Grandma moses(msanii wa vitu asili katika umri mkubwa)
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment