Thursday, 10 July 2014

LOWASSA, SITTA NA WASSIRA HAWANA SIFA ZA KUWANIA URAIS; WARIOBA

 
“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba
“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba
  • Asema anatakiwa awe kijana mwenye maadili, mwajibikaji

  • Asema hatagombea urais, aachwe alee wajukuu

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza Tanzania.

Warioba alisema kwamba taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na vijana wenye nguvu ya mwili na akili. “Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini, unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa utawala wa awamu ya nne.

“Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira, uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa.   Sifa hizi hazipatikani kutokana na uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo,” alisema Makamba.

Alitolea mifano mingi duniani ambapo vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair wakati anakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliongoza nchi hiyo kubwa wakati alikuwa hajawahi kuwa hata Naibu Waziri.

“Barack Obama (Rais wa Marekani) alikuwa Seneta miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa Mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na miaka 39 tu.”

Katika maelezo yake Jaji Warioba alisema kwamba tangu uhuru, walioshika madaraka ya kuliongoza taifa walikuwa ni vijana.

Wazee kugombea urais

Akijibu swali kama atakuwa tayari wananchi wakimtaka kuwania urais baada ya kazi kubwa ya kukamilisha Rasimu ya Katiba nchini, Jaji Warioba alisema:

“Hili nilikwishalijibu, tusahau mawazo kwamba sisi (wazee) tutarudi madarakani. Nadhani mara ya mwisho tulipozungumza niliwaambia inafika wakati kiongozi unang’atuka. Unawaachia vijana ambao wana nguvu ya kimwili na akili ndiyo watumikie taifa hili, waongoze nchi.

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.

Alisema kuwa tangu uhuru hadi sasa Tanzania imetayarisha vijana wengi wanaofaa kuliongoza taifa na kuongeza:

“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”

Huku akitaja mifano ya viongozi hao vijana walioongoza taifa, Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema:

Makundi ya urais

Warioba pia aliulizwa iwapo makundi yanayotajwa kusaka urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuwa huenda yanahusika na kusuasua kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema kwamba, yeye na wenzake waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kutafakari mchakato huo unavyokwenda ukihusisha maeneo na makundi mbalimbali.

“Tulikwenda kutafakari, hatutaki kwenda kwenye matukio, wala kuzungumzia makundi, nasema wote wakae pamoja waone masilahi ya taifa, kwa sababu wasipokaa pamoja kuna hatari ya mchakato huu wa Katiba Mpya kukwama. Na kukwama siyo kwa masilahi ya taifa,”alisema.

Ikiwa Rasimu ya Katiba Mpya itapitishwa na mapendekezo yake ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, kutalazimika kuwapo kwa Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo nguvu na mfumo wa kisiasa kubadilika.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment