Tuesday, 21 October 2014

Wema: Umaarufu hauna faida kwake






Dk. Damas Ndumbaru

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu amesema kuwa kila kukicha yeye anafikiria jinsi ya kupata mafanikio makubwa zaidi kushinda aliyonayo sasa kwani umarufu kwake si kitu cha umuhimu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Wema alisema kuwa umarufu unashida wala hauna faida yeyote ila mafanikio ndio kitu cha umuhimu zaidi na kitu ambacho anafikiria kila siku afanye nini ili aweze kuwa na mafanikio kama waliokuwa nayo mastaa wa kimataifa.

Alisema kuwa anashangazwa na badhi ya wasanii ambao wanaona umaarufu ndio kitu cha muhimu kwao bila ya kujua kwamba kama hauna mafanikio mazuri katika kazi zako umaarufu unaweza ukaja na ukafa kama ilivyo kwa wengine waliopita.

“Mimi siwezi kulingia umaarufu wakati najiona sina mafanikio nitafanya kila mbinu kuweza kupata mafanikio makubwa zaidi ili niweze kuijenga heshima jina langu kwa mashabiki zangu,”alisema

Alisema kuwa kwakwe kitu anachokifikiria zaidi ni afanye nini ili aweze kupata pesa na si kuwaza afanye kitu gani ili umarufu uzidi kwani ukiwa na hela kila kitu kitawezekena ukiwa na uhakika wa kuipata kila uamkapo asubuhi.
TANZANIA CREDIT

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment