Imekaa poa sana! Miezi kadhaa baada ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers kufichua uchafu wa biashara haramu ya ngono kwenye Mtaa wa Mwanzo Mgumu, Kata ya Mwembesongo, maeneo ya Msamvu mjini hapa, warembo wanaojiuza eneo hilo wamekula kibano na malori yanayopaki mahali hapo yametimuliwa.
Baadhi ya machangu walionaswa wakijiuza. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, kiongozi wa mtaa huo, Said Omar Kamba alisema: “Kwanza nayapongeza magazeti ya Global (Publishers) kupitia kitengo chao cha OFM ambao walivamia Kambi ya ltingi (Msamvu) kwa kushirikiana na polisi na kuwafuma wanawake waliokuwa wakifanya biashara haramu ya kuuza miili na kutupa hovyo kondom ambazo watoto wa mtaani kwetu walikuwa wakiziokota na kupuliza wakidhani ni mapulizo, jambo ambalo ni hatari.“Baada ya habari hiyo kuripotiwa na magazeti ya Global, tumewatimua wanawake wanaojiuza baada ya kuketi kikao cha Baraza Maalum la Kata ‘BMK’ na kukubaliana kwamba dawa yao ni kuyaondoa malori eneo hili la ltingi.
Alipoulizwa malori hayo sasa yamehamishiwa wapi, kiongozi huyo alisema: “Tumeyatengea eneo la Njia-Panda ya Tungi nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment