Wanaume ambao ni wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu.
Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.
Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi.
Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.
Waandishi wa waraka huo wa
maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara
nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.
Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi.
Wanafanya hayo, katika mazingira
magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo
wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine na hata
wanawake warefu wanaokutana nao.
Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa,
lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa
kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha.
Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.
Nazo ni, wanaume wafupi
wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa
wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti.
Hali ya kukata tamaa ndio
inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao
pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu
kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu hilo halliwajalishi.
Moja wapo ya ufumbuzi wa ripoti
hiyo pia ni kwamba wanaume wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani
wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume warefu, ingawa utafiti pia
unaonyesha kwa wanaume wenye kimo kirefu, aina ya kazi zao za nyumbani
inatofautiana.
Kwa maana nyengine, wanaume
wafupi hawafiki juu ya makabati. Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa kwa
sababu ya kutaka kuridhisha, bali wanadumu kwenye ndoa kwa sababu
wanataka kuonekana.
Utafitio huu kama ulivyosoma hapo
awali umeua mjadala mkali lakini pindi mtu anaposoma utafiti wao
kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.
Hii ni licha ya mazingira magumu
wanayokabiliwa nayo katika ndoa zao na hufanya hivyo na wake wafupi
waliowaoa lakini pia na wanawake warefu wanaokuwa wamewaoa.
Utafiti huo unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana kasi ya kuoa lakini wanapooa wao hudumu katika ndoa zao.
ANKO SAM BLOG
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook



0 comments:
Post a Comment