Wednesday, 8 October 2014

NAY WA MITEGO ASEMA 'STUNT' YA KUMWAGIA MAJI MASHABIKI SIO AGIZO LA MGANGA




Nay wa Mitego akiwamwagia mashabiki maji

Nay ameiambia Bongo5 kuwa kufanya hivyo ni kuwatia mzuka mashabiki wake na sio kama wengine wanavyotafsiri kuwa ni agizo la mganga. Rapper huyo amesema katika maisha yake hajawahi kwenda kwa mganga.

“Nilijua watu wataanza kuzungumza kuhusu yale maji ambayo nayatumia. Kitu ambacho ninaweza nikasema yale ni maji ya kawaida, sijui ni nini kimenijia kichwani, nikaamua nitumie maji na ninashangaa tu huwa nikitumia maji kuwamwagia watu wanakuwa kama wanapagawa hivi! Mzuka unakuwa juu zaidi yaani sijui ni kwanini inakuwa hivyo. Nimesikia hilo suala, sifanyi hivyo ili kutimiza agizo la mganga na maji ambayo huwaga nayatumia ni yale ambayo tunawekewaga kwaajili ya kunywa. Sijawahi kwenda kwa mganga wala sina chale niliyochanjwa ili muziki wangu u-shine,” amesema Nay.

ANKO SAM BLOG

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment