Mwanamke
mmoja huko mkoani Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata mtoto wake
mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili ya mshikaki.
Mwanamke
huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya unyama huo
mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo alifanya hivyo akiwa
amelewa.
Kamanda
wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo ataendelea
kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika kabla ya
kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI
katika hospitali ya Kibosho mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilofanya
hadi mama yake ambaye ni mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia
kitendo hicho.
Alisema
mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na kumsalimia kisha
akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae aliingia jikoni na
kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake baada ya kumwambia
alishinda na njaa siku nzima.
ANKO SAM BLOG
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:
Post a Comment