Mgeni
rasmi Mhe. Peter Toima Kiroya wa pili kushoto mkazi wa Manyara Wilayani
Simanjiro ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma
akiwaongoza vijana wa kimasai kundi la Korianga kuingia kwenye boma kwa
ajili ya kushiriki sherehe ya unywaji wa maziwa ikiwa ni mojawapo ya
hatua ya makuzi kwa vijana jana mkoani Manyara, wapili kulia ni Mke wa
Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya. 

Mgeni
rasmi Mhe. Peter Toima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani
Kigoma akipokea Kiyabuyu cha maziwa kutoka kwa Mkewe Bi. Filomena Toima
Kiroya kama ishara ya kuwaonyesha vijana waliohitimu hatua moja ya
makuzi katika sherehe za unywaji wa maziwa Mkoani Manyara katika Wilaya
ya Simanjiro.

Mmoja wa
vijana wa kimasai kundi la Korianga akipokea kibuyu cha maziwa kutoka
kwa mke wake kama ishara kuwa kuanzia sasa anaruhusiwa kunywa maziwa
katika boma lake bila ya kujificha kama alivyokuwa akifanya kabla ya
kuingia katika hatua hiyo ya makuzi kwa vijana wa kimasai.

Bw. Onesmo Toima akinywa maziwa
yaliyomo katika kibuyu baada ya kuvuka hatua ya malezi iitwayo Sporio na
kuingia hatua ya Korianga katika sherehe za unywaji wa maziwa
zilizofanyika jana Mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa hotuba wakati wa Sherehe za unywaji
wa maziwa kwa vijana wa kimasai kama hatua mojawapo ya malezi kwa
vijana, kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.


Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment