


Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akivishwa
vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa mkuki na Chifu Mkuu wa
Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya
kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya
Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.
Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya, mkoani Tabora.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na
Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira
wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa mnara wa
kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na
Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira wakiwa
kwenye picha ya pamoja na machifu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini
walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike
Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita. Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment