Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A
wakiwa wamenyoosha mikono juu,kwenye mkutano wa hadhara,wakati Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono jambo Mbunge wa jimbo
la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,katika suala zima la
Utekelezaji wa Ilani ya CCM .
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa
Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao
30,mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole
Sendeka wakati akiangalia josho la ng’ombe la Orkirung’rung ambapo
kuna mradi wa ufugaji wa ng’ombe chotara ambao ni ufugaji wenye tija na
unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka akifafanua jambo Kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),kuhuasiana na Mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa
(Nyama na Maziwa),wakati akiangalia josho la ng’ombe la Orkirung’rung
ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng’ombe chotara,ufugaji wenye tija na
unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Pichani mbele ye bango kulia ni
jengo la Mama na Mtoto la kituo cha Afya Orkesument,Wilayani
Simanjiro,ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikagua.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimsikiliza Dkt.Juma
Nahonyo wakati wa ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika
kituo cha Afya cha Orkesument,kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh
Christopher Ole Sendeka
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha Mazingira kilichopo
mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.Kikundi hicho
kitatumika kueleimisha wananchi wa mji huo katika masuala ya usafi na
kulinda mazingira,kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mambo ya maambukizi
ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa Orkesument kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo wilayani Simanjiro,Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa ahadi za Rais zilizoahidiwa 2010 zitatekelezwa kwa zilivyoahidiwa kwa wananchi wa Simanjiro,pia aliwasisitizia wananchi hao kutochagua viongozi wa vijiji wa hovyo ambao mwisho wa siku ndio wanaoleta mikorogo na migongano kwa wananchi kwa kuuza ardhi,hali inayoleta migogolo isiyokwisha kila siku.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakielekea kukagua jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,wilayani Simanjiro

Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh
Christopher Ole Sendeka akitetea jambo na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Kitwai A,Simanjiro mkoani Manyara.

Mdau akifuatilia jambo

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM,wilayani ya Simanjiro,Ndugu Brown Ole
Suya pamoja na Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka .

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook
0 comments:
Post a Comment