Kiungo wa timu ya Ivory Coast, Geoffrey Die (kushoto) akilia baada ya kupata kipigo kutoka kwa timu ya Colombia siku ya jana.Matokeo hayo yanaifanya Ivory Coast ibaki nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya mechi mbili, wakati Colombia inapanda kileleni kwa pointi zake sita na kujihakikishia kutinga 16 Bora moja kwa moja.
Ivory Coast sasa watalazimika kuifunga Ugiriki katika mchezo wake wa mwisho wa kundi hilo ili kusonga mbele.
Colombia ilipata bao lake la kwanza dakika ya 64, mfungaji James Rodriguez aliyeunganisha kona ya Cuadrado.
Wakati Ivory Coast wanatafuta bao la kusawazisha kwa nguvu zote, shambulizi la kushitukiza liliipa Colombia bao la pili dakika ya 70.
Ivory Coast haikukata tamaa hata baada ya kuwa nyuma kwa 2-0 na iliongeza umakini, ikianza kulinda lango na kushambulia kwa ujanja zaidi. Hali hiyo iliwasaidia kupata bao la kufutia machozi dakika ya 74, mfungaji Gervinho ambaye aliwachambua mabeki wa Colombia kabla ya kufumua shuti lililotinga nyavuni.
Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook



0 comments:
Post a Comment