Wednesday, 18 June 2014

*BRAZIL YAPIGWA `STOP` NA MEXICO DAKIKA 90 ZAMALIZIKA KWA DROO 0-0


 Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar, akisikitika baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo kati yao na Mexico huku timu hizo zikitoka uwanjani bila kufungana pamoja na kila timu kuonyesha kiwango na uwezo na kushambuliana kwa zamu na kila timu ikikosa kosa mabao kadhaa. Hadi mwisho wa mchezo huo Brazil 0-Mexico 0. kwa matokeo hayo sasa katika kundi lao la A timu hizo zimefungana kwa Pointi sawa huku Brazil ikiongoza kwa idadi ya mabao na sasa Brazil anatarajia kukutana na Cameroon.

Kipa wa Mexico, Uchoa, akiruka kuhakiki moja kati ya mpira wa hatari uliopigwa langoni kwake.
Neymar, akimfinya beki wa Mexico....
Hapa ilikuwa ni patashika, nguo kuchanika, mpira uende mtu abaki....

*NI KIPINDI CHA PILI BADO SI BRAZIL WALA MEXICO

 Neymar, akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mexico, wakati wa kipindi cha kwanza, hadi sasa bado ni droo na sasa ni kipindi cha pili.
 Ramiles, akiwatoka mabeki wa Mexico....
 
Nani kuibuka mbabe leo baada ya timu zote hizi mbili kuibuka na ushindi mnono katika mechi zai za ufunguzi??? mwamuzi ni dakika 90.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment