Saturday, 22 November 2014

RAY: CHUCHU SASA NDO’ KILA KITU KWANGU




Stori: Musa Mateja
LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu.

Legendary kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.


Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.

“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’.

Like Page Yetu Hapa Kuungana Nasi Facebook

0 comments:

Post a Comment